Jumapili, 19 Machi 2017

NINI MAANA YA RIBA NA NI YAPI MADHARA YAKE KATIKA JAMII?

        RIBA NA MADHARA YAKE KATIKA JAMII

Image result for riba in islam
- Riba ni kipato chochote kile cha ziada kutokana na mkopo au mtaji bila kushiriki katika faida au hasara.
Rejea Qur’an (2:275-276)

UHARAMU WA RIBA
i. Uislamu umeharamisha riba kwa sababu ni dhulma (unyonyaji) kwa mnyonge mwenye dhiki aliyekopa ili kukidhi haja ya msingi kimaisha.
Uk. 83 kati ya 1 3 1
ii. Riba inahamisha mali na rasilimali kutoka kwa maskini au wanyonge kwenda kwa matajiri.
iii. Riba huondoa usawa na uadilifu katika kugawa na kutumia mali na rasilimali baina ya maskini au wanyonge na matajiri.
iv. Riba imeharamishwa kwa sababu huleta maisha ya kivivu na kutowajibika kwa matajiri, kuchuma bila jasho lolote.
v. Riba ina sababisha watu maskini na wanyonge wabakie kuishi kidhalili kwa kuwatumikia matajiri tu.
vi. Riba husababisha uchumi kuzorota kwa kumikiwa na watu wachache au vyombo kama mabenki, bima, kwa mfumo wa riba.


                                   MADHARA YA RIBA KATIKA JAMII
i. Riba inachafua nafsi ya tajiri, kwa kuwa bahili, mchoyo asiyetayari kuwasaidia maskini, wanyonge na wenye shida mpaka bila malipo yeyote ya ziada.
ii. Riba huchafua mali ya tajiri kutokana na njia haramu za kuchuma na kumiliki bila kuzingatia mipaka.
iii. Riba inakandamiza wanyonge, maskini na wenye dhiki na matatizo, wenye kuhitajia misaada ili waweze kuishi.
iv. Riba inaharibu uchumi na maendeleo ya jamii kwa kudhulumu kundi la maskini na kufaidisha kundi la matajiri.
v. Riba inahamisha uchumi, mali na rasilimali kutoka kwa maskini na wanyonge kwenda kwa matajiri.

Image result for RIBAImage result for riba in islam