Jumatatu, 3 Aprili 2017

JE UNAFAHAMU KAMA UBONGO UNATENGEZWA MCHUZI? soma hii

                   MCHUZI WA UBONGO

Ubongo kilo 1

Vitunguu ½ kilo

Tungule ½ kilo

Samli ¼ kilo

Thomu kiasi

Bizari nzima kiasi

Hiliki kiasi

Pilipili manga kiasi

Mdalasini kiasi

Chumvi kiasi

Tangawizi mbichi kiasi

Limau kidogo (ukipenda)

1                    Uoshe ubongo upachuepachue uweke katika chujio uvuje maji.

2                    Kata vitunguu, saga thomu, tungule pamoja na viungo vyote vilivyobakia.

3                    Teleka sufuria utie samli.Ikichemka tia vitunguu uvikaange mpaka vipige wekundu. Tia tungule ukaange. Kisha tia viungo vyote ulivyovisaga. Mwisho tia ubongo ukaange. Baadae tia chumvi, limau na maji kidogo. Acha uchemke, ukikauka epua.         REFERENCE
click here