MBOGA YA
KISAMVU
Kisamvu
fungu 1 kubwa
Nazi 3
Vitunguu
¼ kilo
Chumvi kiasi
1 Kichambue kisamvu
ukikatekate ukipike mpaka kilainike.
2 Kuna nazi uchuje tui zito zito. Kata vitunguu vyembamba
vyembamba.
3 Maji yakishakauka tia
vitunguu utie na tui upike mpaka tui likauke. kisha epua.
MBOGA YA
KABICHI
Kabichi kilo
1
Vitunguu ½
kilo
Samli ¼ kilo
Mayai 4
Tungule
¼ kilo
Pilipili
manga kiasi
Chumvi kiasi
1 Likate kate kabichi ulioshe
ulpike mpaka liive.
2 Kata vitunguu, katakata
tungule na zisage pilipili manga.
3 Teleka sufuria utie samli,
ikichemka tia vitunguu uvikaange. Tia tungule ukaange, tia kabichi, tia chumvi
na pilipili manga. Kisha vunja mayai uyapige utie. Koroga mpaka likauke. kisha
epua
MBOGA YA
MAGANDA YA MAMUNG’UNYA
Maganda ya
mamung’unya kiasi
Vitunguu ¼
kilo
Tungule ¼
kilo
Mayai 4
Samli kiasi
Chumvi kiasi
Pilipili
manga kiasi
1 Yakate kate maganda ya
mamungunya madogo madogo kama vitunguu, uyapikekwa maji mpaka yaive.
2 Kata vitunguu, ukatekate
tungule na usage pilipili manga.
3 Teleka sufuria utie samli,
ikichemka tia vitunguu uvikaange. Tia tungule ukaange, kisha yatie maganda
pamoja na chumvi na pilipili manga. Vunja mayai uyapige uyatie. Koroga kidogo,
ikikauka epua.
MCHUZI WA
SAMAKI
Samaki kilo
1 (vizuri akiwa nguru)
Vitunguu
maji ½ kilo
Nyanya ½
kilo
Vitunguu
thomu kiasi
Samli ¼ kilo
Mbatata ½
kilo
Mdalasini
kiasi
Pilipili
mbichi kiasi
Bizari nzima
kiasi
Hiliki kiasi
1 Mkate samaki umwoshe. Mtie chumvi na
ndimu mkaange.
2 Kata vitunguu saga tungule, saga
vitunguu thomu pamoja na viungo vyote vilivyobakia. Chemsha mbatata uzimenye.
3 Teleka sufuria utie samli. Ikichemka
tia vitunguu maji uvikaange. Vikianza kupiga wekundu tia tungule. Kisha tia
viungo vyote ulivyovisaga. Halafu tia mbatata na baadae utie vipande vyote vya
samaki. Tia ndimu, chumvi na maji kidogo. Wacha vichemke kidogo. Onja ukiona
kila kitu sawa, epua
REFERENCE
click here
REFERENCE
click here