WALI WA
CHOOKO
Mchele kilo1
Chooko ½
kilo
Samli kiasi
Nazi 2 nzuri
Vitunguu
thomu kiasi
Bizari nzima
kiasi
Vitunguu
maji kiasi
Hiliki kiasi
Mdalasini
kiasi
Chumvi kiasi
Karafuu
chembe 2 au 3
1 Osha mchele pamoja na
chooko uweke pembeni.
2 Kuna nazi uchuje tui kama
la wali wa nazi uliweke.
3 Menya vitunguu maji,
uvioshe uvikate uviweke. Menya vitunguu thomu uvitwange pamoja na bizari na
hiliki. Osha vijti vya mdalasini na chembe za karafuu uziweke.
4 Teleka sufuria utie samli,
ikichemka tia vitunguu uvikaange. Baadae tia viungo vyote ulivyovitwanga utie
na chembe za karafuu pamoja na vijiti vya mdalasini. Kisha tia tui la nazi.
Likianza kufumba tia mchele pamoja na chooko zake utie na chumvi. Acha utokote
mpaka wali ukauke. Ukishakauka funika upalie moto.
REFERENCE
click here
REFERENCE
click here