Kuamini Qadar ya Allah (s.w)
o Maana ya Qadar
Kilugha: maana yake ni kipimo, kiasi au makadirio.
Rejea Qur’an (54:49), (25:2),
(36:39).
Kisheria: ni mpango (plan) wa Allah (s.w) unaohusu kutokea,
kuwepo na hatima ya maumbile na viumbe vyake vyote na matukio yatakayopelekea
kutokea na kuondoka kwake.
Rejea Qur’an (57:22), (6:59)
o Maana ya Qudra
Ni uwezo wa Allah (s.w) usio na
mipaka katika kufanya chochote na lolote atakavyo kwa kuliambia “kuwa” na
linakuwa.
o Umuhimu wa Kuamini Qadar ya Allah (s.w)
(i) Kuamini Qadar ya Allah
(s.w) ni nguzo ya sita katika nguzo za imani ya Kiislamu.
(ii) Kuamini Qadar ya Allah
(s.w) kikweli kweli ndio msingi wa imani sahihi ya muumini juu ya mipango na
uwezo wa Allah (s.w).
(iii) Kutoamini Qadar ya Allah
(s.w) ni miongoni mwa makosa yatayoharibu itikadi ya mja juu ya utendaji na
mwenendo wake.
(iv) Hakuna chochote
kitakachofanyika au kutokea kwa viumbe isipokuwa kimeandaliwa na kupangwa na
Allah (s.w).
o Mtazamo wa Uislamu juu ya Qadar
a) Ni makosa makubwa kudhani
kuwa mtu anaweza kufanya jambo lolote lile kinyume na Qadar ya Allah (s.w).
b) Ni makosa makubwa mtu
kumlaumu Allah (s.w) kwa maovu anayoyatenda kuwa ndiye amemkadiria kuyafanya.
Uk. 23 kati ya 1 3 1
c) Allah (s.w)
anayajua yote atakayoyafanya mja hadi hatima ya maisha yake siku ya Qiyama hata
kabla ya mtu huyo hajazaliwa.
Rejea Qur’an
(11:6)
d) Isidhaniwe
kuwa maadamu mtu amechagua kumuasi Allah (s.w) basi Allah (s.w) hana uwezo wa
kumzuia, bali atafanya hivyo tu iwapo lipo katika Qadar ya Allah.
e) Utatanishi
wa Qadar huondoka kwa kuzingatia maeneo makuu mawili;
i. Eneo la
hiari (uhuru) ambalo mtu huchagua kufanya jambo jema au baya atakalo.
ii. Eneo
lisilo la hiari kwa mtu kuamua kufanya jambo lolote atakalo, mfano; kuchagua
wazazi wa kumzaa, sehemu, muda wa kuzaliwa, jinsia, n.k.
f) Mtu
ataulizwa au ataadhibiwa kwa matendo ya hiari tu ambayo ana uhuru nayo wa
kuchagua lipi afanye na lipi asifanye.
g) Mwanaadamu
hataulizwa kamwe matendo yasiyokuwa hiari kwake, mfano; kwa nini aliumbwa
mweusi, mrefu, wa kike, wa kiume, kabila au nchi fulani, n.k.
o Kueleweka
vibaya kwa Qadar na Qudra ya Allah (s.w)
Baadhi ya
Waislamu na watu wengine wanapotosha maana na nafasi ya Qadar na Qudra ya Allah
(s.w) kama ifuatavyo;
i. Kuacha
kutekeleza wajibu wao kwa Allah kwa kusingizia kuwa “imeshaandikwa kwenye
kitabu cha Allah kuwa sisi hatutatekeleza au tutatekeleza jambo fulani”
ii. Baadhi ya
watu wanaojiita waislamu kuacha kutekeleza amri za Allah (s.w) kama swala,
funga, n.k. kwa kusingizia kuwa hawajajaaliwa kufanya hivyo na watatekeleza
pindi watakapojaaliwa.
iii. Baadhi ya
watu, miongoni mwa waislamu hufanya maovu kwa shangwe kwa kudai kuwa hivyo
ndivyo alivyokadiriwa na Allah (s.w) na wasingeweza kukwepa Qadar yake.
Uk. 24 kati
ya 1 3 1
iv. Baadhi ya
watu kudai kuwa, “Allah (s.w) mwenyewe ameshajua na ameshapanga kuwa watu wa
motoni au peponi, hivyo hakuna haja ya wao kufanya uovu au wema”.
v. Watu
wengine wanadai kuwa, “Allah (s.w) amewapendelea wengine kwa kuwapangia kwenda
peponi huku akiwadhulumu wengine kwa kuwapangia kwenda motoni.
Madai haya
hutiliwa nguvu hata kwa ushahidi wa aya za Qur’an kama ifuatavyo;
Rejea Qur’an (39:36-37), (29:62), (2:284), n.k