NAMA YA KUKABILIANA NA MAFUA.
Mafua ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vya mafua na pia inasadikika kuwa zipo takribani aina
200 za virusi hawa wa mafua wakiwemo
rhinoviruses, parainfluenza
viruses, enteroinfluenza viruses na vingine vingi. Virusi hivi hupatikana kwa kukutana
na hewa yenye virusi hawa, pindi unapovuta hewa yenye mchanganyiko wa virusi
hawa. Sababu zingine zinazosadikika kusababisha mafua ni panoja na sigara,
moshi, mavumbi, baridi kuwa kali au kuchafuka kwa hewa.
Udonjwa wa mafua unadalili tofauti tofauti na huenda zikafanana na ugonjwa
wa malaria. Miongoni mwa dalili hizo ni pamoja na kukosa hamu ya kula, kuhisi
uchovu, kutokwa na makamasi mengi, koo kukereketa, maumivu ya kichwa na kupiga
chafya mara kwa mara. Japo dalili za mafua hutofautiona kwa mtu na mtu
kulingana na uwezo wa mwili wake kupambana na magonjwa ila hizi dalili tulizozitaja
huwa maarufu kwa watu wengi.
Mgonjwa wa mafua huenda akawa amechoka sana kiasi kwamba analala kitandani
kwa homa kali aliyo nayo. Mafua huwaathiri zaidi watoto na wazee kwani miili
yao haina kinga za kutosha kupambana na maradhi. Kwa wale wenye HIV+ ugonjwa wa
mafua pia hueza ukawaletea athari kubwa sana ikiwemo homa kali na uchovu.
Mtu ana weza kujikinga na mafua kwa kuosha mikono kabla na baada ya
kula, kuziba mdomo anapopiga chafya.
Kula vyakula vyenye vitamin A na C kwa wingi, kunywa maji mengi na kupunguza
mawazo yaani ”stress” kwa lunga ya
kigeni hapa kinacho maanishwa ni kuwa na furaha. Jambo la msingi limgine ni
kuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi mara kwa mare humuepusha mtu na mafua kwa
kiasi kikubwa.
Miongoni mwa vyakula anavyotakiwa ale mwenye mafua ni kama mboga za
majani zenye vitanimi kwa wingi, kwa
mfano spinach, na mchicha. Pia kula matunda yenye vitamin C kwa wingi kama
mapapai, na machungwa. Vyakula hivi husaidia katika kuupa mwili uwezo mkubwa wa
kupambana na maradhi na mashambulizi mengine. Maji ya kutosha humsaidia mtu
mwili wake kuweza kufanya kazi ya kudhibiti maambukizi kwa urahisi. Hali
kadhalika kufaya mazoezi husaidia mwili kufanya kazi vizuri. Pia anashauriwa
mgomjwa wa mafua awe chai.
Wapo baadhi ya wataalamu wa tiba mbadala wanazungumzia matumizi ya kitunguu
maji kuhusu kutibu mafua. Wanatumia harufu ya kitunguu maji kutibu mafua.
Mgonjwa atachukuwa kitunguu kasha ataondowa majani, au maganda ya juu kisha
atakuwa anavuta haruvu ya kitungu. Atafanya hivyo kwa mara kadhaa hasa
anapokwenda kulala.