SHIRK
1.1.
Shirk.
·
Maana : Shirk
ni kinyume cha Upweke au Umoja (Tawhiid)
·
Maana ya
Kumshirikisha Mwenyezi Mungu (s.w):
Ni kujaalia kinadharia au kiutendaji kuwa kuna miungu wengine
wanaoshirikiana na Mwenyezi Mungu (s.w) katika kuongoza na kuendesha Ulimwengu.
§ Aina za Shirk.
Kuna aina kuu nne za shirk,
1.
Shirk katika Dhati ya Mwenyezi Mungu – (Shirk
fiy Dhaat).
2.
Shirk katika Sifa za Mwenyezi Mungu – (Shirk fiy
Sifaat).
3.
Shirk katika Mamlaka ya Mwenyezi Mungu – (Shirk
fiy Ikhtiyaar).
4.
Shirk katika Hukumu za Mwenyezi Mungu – (Shirk
fiy Ah-kaam).
1. Shirk katika Dhati ya Mwenyezi Mungu (s.w).
Ni kujaalia au kuvinasibisha viumbe na uungu kwa kuvipa majina rasmi kama
washirika wa Mwenyezi Mungu (s.w) na kuviendea kwa unyenyekevu na ibada maalum
kama, kuvisujudia, kuchinja na kuviomba msaada.
Rejea Qur’an (25:2-3), (22:73) na (29:41).
2.
Shirk katika Sifa za Mwenyezi Mungu (s.w).
Ni kuwasifu au kuwatukuza viumbe kiwango anachostahiki kusifiwa au
kutukuzwa Allah (s.w) peke yake. Kama kuomba
dua, baraka na msaada kupitia kwa Wacha-Mungu, mfano kwa baraka za Mtume,
Abdul-Qadir, Sharifu au Sheikh fulani n.k.
Rejea Qur’an (53:32), (10:62-64), (2:180), (17:110) na
(40:60).
3.
Shirk katika Mamlaka ya Mwenyezi Mungu (s.w).
Ni kuwakabidhi viumbe mamlaka kamili ya Mwenyezi Mungu (s.w) na kuwatii
kwayo kama vile kuongoza, kulisha, kulea,
kulinda n.k katika maisha ya kila siku kinyume na nafasi au uwezo wao.
Rejea Qur’an (9:31) na (2:208).
4. Shirk katika Hukumu za Mwenyezi Mungu
(s.w).
Ni kutunga sheria au hukumu kinyume na sheria au hukumu za Mwenyezi Mungu
(s.w) alizoziainisha katika vitabu vyake vitukufu na kuzitumia kuhukumu kwazo
katika uendeshaji wa maisha ya kila siku.
Rejea Qur’an (5:38), (24:2), (33:36), (5:44-45, 47) na
(5:50).
§
Kina cha
Uovu wa Shirk.
o
Ni dhulma kubwa kuliko zote na ndio chanzo cha
matatizo yote ulimwenguni.
Rejea Qur’an (31:13) na (10:35-36).
o
Ni dhambi kubwa kuliko zote isiyosameheka ila
apende Mwenyezi Mungu (s.w) na kutubia kikweli kweli kabla ya kufa.
o
Ni dhambi inayofuta mema yote ya mtu
aliyoyafanya kabla ya kushirikisha.
Rejea Qur’an (4:48), (4:116) na (39:65).