FAHAMU UGONJWA
WA KISUKARI
kisukari ni ugonjwa unaotokea pale ambapo mwili unashindwa kuzalisha kabisha homon ya
insulin au kushindwa kuzalisha homon hii kwa kiwango kinazotosha. Wakati
mwingine kisukari kinatokea pale mwili unaposhindwa kutumia insulin
inayozalishwa mwilini. Hii ni homon ambayo inakazi ya kuthibiti kiwango cha
sukari ndani ya mwili kisiwe kikubwa au kuwa kidogo. Homoni hii huzalishwa na
kongosho (pancreas.
Kuna aina kuu mbili za kisukari ambazo ni TYPE 1 DIABETS na
TYPE 2 DIABETS. Hii aina ya kwanza ambayo ni type 1 diabets hutokea pale ambapo
mwili unashindwakabisa kuzalisha homon ya insulin. Hii hotokea pale ambapo
mfumo wa afya unaposhambulia na kuuwa homoni ya insulin. Maranyingi aina hii ya
kisukari huwapata watoto na walio na umri kati ya miaka 10-20. Watu wazima
huenda kuwa na kisukari aina hii ila ni kwa uchache. Aina hii ya kisukari
husababishwa na gene (genetic mutationr), au katika mazingira kama mashambulizi
ya virusi.
Aina ya pili ya kisukari type 2 diabets hutokea pale ambapo
mwili unazalisha insulin ambayo si yenye kutosheleza. Au hutokea pale seli za
mwili zinapowacha kutumia hmon ya insulin (insulin resistance). Aina hii ya
kisukari huwapata watu wakubwa ila kwa uchache hueza pia ukawapata watoto. Aina
hii ya kisukari huweza kusababishwa na
kuwa na uzito usio wa kawaida (over weight), umri (kuanzia miaka 45),
kurithi kutoka katika familia/ukoo rangi (race/ethinick background),
kutokufanya mazoezi, vyakula,.
Dalili za kisukari hutofautiana japo wataalamu wa afya
wanataja hizi;-kuhisi njaa kali, kuhisi kiu kikali sana, ngozi kukauka,
kupunguwa kwa uzito bila ya sababu, kukojoakojoa, kutokuona vizuri, kuchelewa
kupona majeraha, kuchoka sana(kuhisi uchovu usio wa kawaida).na kupata ganzi.
Japo kuwa ugonjwa wa kisukari ni hatari kwa afya lakini mtu
anaweza kuishi vizuri kama atafata utaratibu na kanuni nzuri za kuishi na
ugoonjwa huu. Kwa mfano nchini marekani zaidi ya watu milioni 23 wanasumbuliwa
na kisukari lakini wanaishi maisha mazuri tuu. Hivyo kama mgonjwa atafata
kanuni na masharti pamoja na kubadilisha fife style yaani namna anavyoishi
anaweza kupunguza athari za uginjwa huu. Hapo chini utaona ushauri juu ya
mwenye kisukari aishi
Chakula; mgonjwa wa isukari anatakiwa ale chakula kisicho na
mafuta mengi, ckisicho na chumvi wala sukari nyingi. Kuala matunda na mboga za
majani. Hakikisha unakula katika muda maalumu siku zote pia angalau upate
chakula mara tatu kwa siku kula chakula kisicho kobolewa. Pia hakikisha
unakunywa maji mengi zaidi kwa siku
Mazoezi; hakikisha unafanya mazoezi si chini ya mara tatu kwa
wiki. Hii huenda ikasaidia kupunguza usito na kuthibiti kiasi cha sukari ndani
ya mwili wako. Pia kufanya mazoezi ni muhimu
kwa afya yako kwa ujumla. Mazoezi yanaweza kupunguza mlundikano wa
mafuta kwenye ngozi na mishipa yta damu. Hali hii itakusaidia kupunguza
uwezekano wa kuapata strock na shambulio la moyo.
Dhibiti uzito wako; hakikisha kuwa hauna uzito usio wa
kawaida. Yaani hakikisha kuwa unapunguza uzito kama uzito wako ni mkubwa. Pata
ushauri wa daktari kuhusu uzito wako kama unakufaa au umezidi kulingana na afya
yako. Zipo njia nyingi za kupunguza uzito kupitia vyakula, mazoezi na
nyinginezo. Muone daktari au pata ushauri kwa walio na ujuzi wa njia salama ya
kupunguza uzito.
Tumia dawa; kama kisukari kimeshindikana kuthibitiwa kwa nyia
hizo hapo juu anza kutumia dawa. Zipo dawa maalumu kwa wagonjwa wa kisukari.
Pia inashauriwa kuwa mtu aanze kutumia dawa za kumeza kabla ya zile za sindano.
Muone daktari atakupatia dawa hizo kulingana na afya yako. Watu wengi wanakuwa
wavivu wa kunywa dawa lakini kwa baadhi ya magonjwa uvivu huu ni hatari zaidi
kwa afya zao.
Ugonjwa wa kisukari usipopata matibabu mapema au usipo fata
ushauri jinsi ya kuishi na ugonjwa huu matatizo mengi yanaweza kutokea ikiwemo
presha, shambulio la moyo na kupapalaiz (strock), matatizo ya macho na upofu
pia na matatizo ya meno na finzi. kwa ujumla afya ya mtu inaweza kuwa katika
hali mbaya zaidi na pia huenda ikamsababishia kifo.
Hutokea wakati mengine mgonjwa mwenye kisukari sukari
inashuka chini kabisa, hapa mgonjwa anaweza kuonesha dalili mbalimbali
zikiwemo;- kutoka na jasho jisngi,kupiga myayo mara kwa mara, kushindwa
kuzungumza na kushinda kufikiri vizuri, kukosa fahamu, kukosa nguvu hata kidogo, kupata uchovu usio
wa kawaida pia mtu anaweza kujihisi kama ndo anataka kufa vile. Hali ikiwa hivi
kuna huduma ya kwanza ambayo anatakiwa afanyiwe kama kupewa juisi ya matunda
nusu kijombe. Glucose vijiko 3, maziwa kikombe kimoja,
Katika magonjwa yanayosumbuwa leo kisukari ni moja wapo japo
halichangii kuuwa watu wengi kama magonjwa mengine. Ni vizuri kujuwa kama
unakisukari au huna ili uweze kuchukuwa
hatuwa mapema. Pia kwa wale wanaovuta sigara kisukari ni hatari na tabia hii,
ni vizuri kuacha uvutaji wa sigara na kuacha
kabisa pombe kwa ni yote haya ni hatari zaidi kwa mwenye kisukari.