LISHE KULINGANA NA MAKUNDI
YA WATU.
Kila mtu anatkiwa ale chakula kwa kulingana na mahitaji ya
mwili wake. Motto anatakiwa ale vyakula maalumu kwa ajili ya kumuwezesha kukuwa
vizuri umbo na kiakili. Halikadhalika mama wajawazito wanatakiwa wale vyakula
maalumu kwa ajili ya kuwezesha afya ya mama na motto. Wazee, vijana,
wafanyakazi na wagojwa wanatakiwa wale vyakula kulingana na hali zao. Hapa
tutakuletea lishe kwa kulingana na makundi ya watu.
watoto
wanatakiwa kula vyakula vya protini kwa wingi ili
kuwezesha ukuaji wao wa mwili na tishu. Upungufu wa protini unaweza kumpelekea
mtoto awe na ukuaji hafifu. Kwa ukuaji mzuri wa meno na mifupa mtoto anatakiwa
apewe vyakula vya madini kama madini ya kashian(calcium) upungufu wa madini
haya huenda mtoto akawa na ukuaji mbaya wa mifupa. Madini ya zink ni muhimu pia
katika ukuaji wa mtoto.
Vitamini B12 ni muhimu kwa ajili
ya kuhakikisha utengenezwaji wa seli nyekundu za ndamu. Pia ijulikane kuwa
ukuaji mzuri wa mtoto unategemea kuwepo
na damu ya kutosha mwilini ili kuweza kusafirisha gesi ya oxygeni pamoja na
viinilishe(nutrients) ndani ya mwili.
Vitamini ni muhimu sana katika
ukuaji wa mtoto. Watoto wapewe vyakula vyenye vitamini C kwa wingi kama
machungwa, mapapai. Vitamini hivi vinamuwezesha mtoto kutengeneza kinga ya
mwili ili kuweza kupamabana na maradhi.
Watoto pia wanatakiwa wapewe
vyakula vya wanga kwa wingi ili waweze kupata nguvu ya kutosha kuweza kufanya
shughuli zao kama mazoezi ya kutambaa, kukumbia, kusimama n.k.
Wamama wajawazito na
wanaonyonyesha.
Wanaonyonyesha na wajawazito
wanahitaji kupata vyakula vyenye viinilishe vya kutosha ili kuwezesha ukuaji wa
mtoto tumboni , utengenezwaji wa maziwa na kwa ajili ya afya zao wenyewe.
Vyakula vya protini vinahitajika
kwa mkiwango kikubwa ili kuwezesha mwili wa mama kujenga misuli vizuri , tishu
katika mwili wake na mwili wa mtoto aliye tumboni. Utengenezwaji wa maziwa ,
usafirishwaji wa damu na ukuaji wa viungo vya mama na mtoto unahitaji protini.
Hivyo wamama hawa wapewe protini kwa wingi.
Vyakila vya folic asid na
vitamini B vinahitajika kwa ajili ya kuwezesha kupunguza tatizo la kushindwa
kujifunguwa kwa njia ya kawaida. Vyakula vya madini ya kashiam(calcium) ni
muhimu kwa ukuwji wa mifupa ya mtoto aliye tumboni na kuimarika mwili wa mama
pia. Kwani mjamzito asipopewa madini haya mtoto atatumia madini yaliyomo kwa
mama na kumfanya mama awe na mifupa dhaifu katika kipindi hiki.
Madini ya chuma ni muhimu katika
utengenezwaji wa damu, halikadhalika mtoto anahitaji madini haya ili ayatumie
katika wiki ya kwanza ya kuzaliwa. Madini ya zink ni muhimu katika kuwezesha
kujifunguwa.(progression of labour) na ukuaji salama wa mtoto aliyoko tumboni.
Wamama wajawazito wapewe vyakula
vyenye kambakamba (dietary fiber}. Hivi vitamuwezesha kutopata tatizo la kukosa
choo.
Vijana
Vijana wanatakiwa wale sana
vyakula vya kuupa mwili nguvu yaani vyakula vya wanga. Pia wale kwa wingi
vyakula vyenye protini na madini ya chumvuchumvu kama kashiam(calcium), chuma
na phosphorous. Vijana wa kike wanatakiwa wale zaidi vyakula vyenye madini ya
chuma ili waweze kuwa na damu ya kutosha hususan wakati wa vipindi vyao.
Wazee
Wazee hawahitaji kuwewa vyakula
vya kutia nguvu kwa wingi. Wapewe vyakula vyenye kambakamba ili kuwapunguzia
tatizo la kukosa choo na kuwezesha mmeng’enyo wa chakula.
Wazee wapewe vyakula vyenye
madini ya chuma, zink na kashiam(calcium) ili kupunguza uwezo wa kupata tatizo
la anaemia. Pia madini ya zink ni muhimu katika kuufanya mwili uweze kujenga
kinga ya mwili (immune system) na kusaidia kupona kwa urahisi na haraka kwa
majeraha.
Ili kupunguza tatizo la kuchoka
kwa mifupa (mifupa kuwa dhaifu) kwa wazee wanatakiwa wapewe vyakula vyenye
vitamini D na madini ya kahiam(calcium) kwa wingi.
Pia wazee wapewe vyakula ambavyo
ni rahisi kutafuna na kumeza. Hii ni kwa sababu wazee wao huwa meno na mifupa
yao ni midhaifu pia wana upungufu wa uzalishaji wa mate midomoni mwao kwa mfano
baada ya kuwapa nyama wapewe maini.
Wagonjwa.
Wagonjwa wapewe vyakula vyenye
viinilishe vyote ili kuwezesha miili yao kuwa na uwezo mkubwa wa kupambana na
maradhi.
Matunda na mboga za majani ni
muhimu kwa wagonjwa iliwaweze kupata madini na vitamini muhimu kwa ajili ya
miili yao. Wagonjwa pia wapewe maji ya kutosha ili kuwezesha miili yao kufanya
kazi vizuri.
Matunda yatamuwezesha pia
kupambana na maradhi au kupunguza uwezekano wa kuendelea kuuguwa. Wagojwa
wapate muda wa kutosha kwa ajili ya kulala na wafanye mazoezi kulingana na hali
zao.