Chakula bora ni muhimu kwa afya yako. Ulaji mzuri wa chakula
unaweza kukuondoshea madhara na hatari za baadhi ya magonjwa. Ulaji mzuri wa
chakula utaweza kuupa mwili wako kunga
ya kupambana dhidi ya maradhi na mashambulizi mengine. Halikadhalika ulambaya
wa chakula unaweza kuleta hatari ndani ya mwili wako kama vile magonjwa ya
kisukari na saratani.
Mtu anatakuwa kuala chakula bora na si chakula chochote kile.
Mlo kamili huzingatiwa pale mtu anapokula mlo ambao una ndani yake virutubisho
muhimu vinavyohitajika mwilini. Virutubisho hivi ni maji, protini, fat na
mafuta pamoja na madini. Virutubisho hivi vinafanya kazi mbalimbali ndani ya
mwili zikiwemo kulinda mwili, kujenga na kukarabati mwili pamoja na kuutibu mwili.
Vyakula vya protini
Hivi ni vyakula ambavyo vinakazi
ya kuujenga mwili pamoja na kuukarabati mwili. Kupona kwa vidonda na makovu
vyote ni kazi ya protini. Uotaji wa nywele mpya pamoja na kukuwa kwa kucha
baada ya kuzikata vyoye hivi hufanyika shukrani kwa vyakula vya protini.
Unaweza kuvipata vyakula vya
protini kutokana na maziwa, nyama, mayai, na samaki. Katika mimea pia unaweza
kupata protini kwa kula maharage, mchele na baadhi ya nafaka zingine. Pia ulaji
wa mboga za majani unaweza kusaidia kupatikana kwa protini.
Vyakula vya fat na mafuta
Vyakula vya fati husaidia katika
kuupa mwili nguvu. Fat husaidia kulinda seli zilizomo mwilini zisizurike.
Vyakula hivi huupa mwili joto hususan wakati wa baridi. Na inashauriwa wakati wa
baridi kula vyakula vya fat kwa wingi ili kuupa mwili joto. Vyakula vya fat pia
husaidia kuganda kwa damu pindi mtu anapopata jeraha.
Vyakula vya fati ni maziwa,
mafuta ya wanyama, mayai na nyama. Pia katika matunda fat inapatikana kwa wingi
pia kwa mfano katika avocardo, olive, karanga , alizeyi pamoja na mafuta ya
mimea yaani vegetable oil. Samaki ni chanzo kizuri cha fat.
Vyakuala vya vitamin na madini
Mwili unahitaji vyakula hivi ili
uwezesj\he matumizi ya vyakula vingine yawe mazuri tunahitaji viyamini kwa
kuulinda mwili dhidi ya magonkwa. Vitamin c hujulikana kwa kusaidia ugonjwa wa
scuvy ugonjwa huu humfanya mtu atoke samu mwenue mafinzi. Vitamin A husaidia
kurekebisha afya ya macho. Vitamin K husaidia kuganda kwa damu unapopata jeraha.
Mwili unahitaji madini pia ili
uweze kujikinga na hatari zingine. Madini ya chuma ni muhimu katika kujenga
seli nyekundu za damu.madini ya calcium ni muhimu kwa afya ya mifupa na meno
Madini na vitamin hpatikana zaidi
kwenye mboga za majani, na matunda.
Matunda yenye uchachu kama limao, chungwa husaidia kwa vitamin C na mapapai pi
hujulukana kwa kuwa na vitamin C. spinachi ni muhimu kwa vitamin A. samaki
husaidia kwa madini menhine.
Vyakula vya wanga
Vyakula vya wanga ndio vyanzo vikuu
vya nguvu ndani ya mwili. Vyakula hivi hupatikana kwenye starch. Mwili unatumia
vyakula vya wanga katika hali ya glucose. Ambayo huenda maeneo mengine ya mwili
kwa ajili ya kuzalisha energy.
Unawza kupata wanga kwa kula
nafaka kama maharage, matama, mihogo. Pia asali, miwa na viazi ni vyanzo vizuri
vya wanga.
Maji
Zaidi ya 70% ya mwili wa binadamu
ni maji. Tunahiyaji maji ili tuweze kuishi. Mmaji ni muhimu kwa afya. Mtu
anahitaji kunywa maji bilauri 8 mpaka 10
za maji. Mtu anaweza kuishi siku ziaizopungua 8bila kunya maji lakini anaweza
siku nyingi zaidi bila ya kutokula chakula.
Maji husaidia kurekebisha mifumo
mbalimbali ndani ya mwili kama vile mfumo wa utoaji takamwili, mfumo wa chakula
na mfumo wa damu. Maji husaidia katika kutibu maumivu ya kichwa amabayo
yamesababishwa na unywaji mchache wa maji.
VYAKULA VYA KAMBAKAMBA
Hii si katika aina vya virutubisho. Hivi ni vyakula ambavyo
husaidia katika msukumo wa chakula tumboni. Husaidia katika kufanya haja kubwa
itoke kwa usalama. Matatizo ya kuziba kwa choo au kupata hajakubwa kwa kiasi
kidogo husababishwa na kutokula vyakula vyenye hali hii kwa kiwango kinacho
hitajika.
Tunaweza kupata roughage kwenye nafaka zote zisizo kobolewa,
matunda, maharage, kabichi spinach, mihogo na nyanya sikisizo menya na jamii
zingine za vyakula hivi.