SABABU
ZA UGONJWA WA KISUKARI
Ugonjwa wa kisukari ni ugonjwa unaotokea pale ambapo mwili
unaposhindwa kuzalisha homon za insulin au mwili kushindwa kuzalisha homon za
insulin za kutosha au mwili kushindwa kutumia homon za insulin. Wakati mwingine
hutokea pale mfumo wa kinga mwilini
(immune system) unapoathiri organ ya pancrease na kuathiri uzalishaji wa homon
ya insulin.
Ugonjwa wa kisukari husababishwa na mabo mengi yakiwepo
kurithi kutoka kwenye familia, mazingira na ufumo mbaya wa maisha (life style).
Japkuwa ugonjwa wa kisukari huweza kurithi kutoka kwa wazazi au familia lakini
mfumo mbaya wa maisha huchangia kwa kiasi kikubwa pia katika kusababisha ugojwa
huu wa kisukari. Katika post hii nitazungumzia kwa namna gani mfumo mbaya wa
maisha unavyoathiri kupatikana ugonjwa wakisukari.
1.
Kuzidi
uzito mwilini; kikawaida mwili unahitaji uzito maalumu kulingana na kanuni za
afya. Uzito ukiwa mkubwa sna ni tatizo na ukiwa ni mdogo sana pia ni tatizo.
Uzito kuwa mkubwa zaidi unapelekea homon ya insulin kutokuzalishwa kiwango
kinacho takiwa au mwili kushindwa kutumia insulin vizuri (insulin resistance).
Zipo njia nyingi za kupunguza uzito zikiwepo kupitia vyakula, mazoezi au
kubadilisha mfumo wa maisha. Hakikisha kuwa uzito wako upo katika hali ya
kawaida. Muone daktari akupe ushauzi kuhusu uzito wako.
2.
Kutokufanya
mazoezi; kikawaida mazoezi yana faida kubwa sana mwilini, zikiwemo kuufanya
mwili uwe imara. Mazoezi huweza kusaidia mifumo mbalimbali ya mwili kufanya
kazi vizuri kama vile mfumo wa chakula, mfumo wa damu na mfumo wa afya. Mazoezi
huweza kumkinga mtu na magonjwa ,mbalimbali kama vile mafua, presha ya damu,
shambulio la moyo na kisukari. Mazoezi hupunguza mlundikano wa mafuta kwenye
mwili na kusaidia kuondowa uchafu mwilini kwa njia ya jasho. Kiafya inashauriwa
mtu afanye mazoezi japo kwa wiki asikose mara tatu. Yapo mazoezi mengi tuu na
yasiyo na haja na kujiumiza saana kama vile kuruka kamba au kukumbia jogging.
3.
Mpangilio
wa lishe, chakula ni muhimu kwa maisha ya kiumbe chochote, ila ulaji mbaya pia
ni tatizo kwa afya ya kiumbe pia. Mtu anatakiwa ale chakula kwa namna ambayo
haitamletea madhara katika afya yake. Mtu anatakiwa ale chakula ambacho
hakitamletea kuzidi uzito au utapia mlo au kitambi. Haya huenda yakawa na
madhara katika afya ya mtu na hatimaye kupata kisukari. Chakula chenye mafuta
mengi, sukari nyingi ama chumvi nyingi vyote sio vizuri kutumia.
4.
Mazingira; wakati mwingine inatokea mazingira
watubwanayoishi yakapelekea kupata kisukari kwa mfano mashambulizi ya virusi. Kuna aina ya virus
ambao wanashambulia mwili na kufanya mwili kushindwa kusazalisha homoni za
kutosha kwa ajili ya kushibiti kiwango cha sukari ndani ya damu.
5.
Kutithi;
unaweza kupata ugonjwa wa kisukari kwa njia ya kurithi kutoka katika familia.
Kama ilivyo kwa magonjwa mengine ya kurithiwa kwa kupitia vizazi au kurithi
rangi ya ngozi urefu au ufupi kutoka kwa wazazi vivyo hivyo kisukari huweza
kurithiwa. Haijalishi kati ya baba nani ana kisukari lakini huenda ukakipata
kwa kurithi. Pia huenda wazazi wakakwa na kisukari na wewe ukakisosa pia.
Hitimisho
Ijapokuwa
ugonjwa wa kisukari ni hatari sana lakini kama mtu atafata masharti anaweza
kuishi maisha mazuri tuu kama watu wengine. Jambo la msingi hapa ni kufuata
masharti na kuendelea kutumia dawa za kisukari . Kufanya mazoezi na kubadilisha
utaratibu wa chakula.