VIJUE VYAKULA VYA VITAMINI NA FAIDA ZAKE
Vitamin ni muhimu katika kuhakikisha kuwa mwili unatumia
virutubisho vingine kufanya kazi zake. Kuna vitamin A,B,C,D,E na K. vitamin B
vimegawanyika katika makundi kama vitamin B1,B2,B6, na B12. Ukosefu wa vitamin vyovyote
kati ya hivi unaweza ukapelekea matatizo makubwa kwa afya ya mtu.
Vitamin A,D,E na K, vinaitwa fat soluble vitamin. Hivi
nhuweza kuhifadhiwa ndani ya mwili. Hivyo hatuhitaji kula vyakula kuvipata kwa
kila siku. Kwa upande mwengingine vitamin B na C huitwa water soluble vitamin,
hivi havihifadhiwi ndani ya mwili, hivyo tunahitaji kula vyakula vyenye vitamin
hivi kwa kila siku.
Vitamin A hupatikana kwenye maziwa, maini, karoti,machungwa,
na mboga za rangi nya njano.. vitamin hivi ni muhimu kwa kusaidia afya ya macho
na mfumo wa upumuaji (respiratory track). Ukosefu wa vitamin hivi unapelekea
mtu kushindwa kuona wakati wa usiku. Mwili unakuwa ni rahisi kupata mashambulio
pindi mtu akiwa na vitamin A kwa uchache.
Vitamin B1 hivi
hupatikana kwenye nyama, maini, mayai,hamira na mchele. Husaidia katika
kuhakikisha michakato ya kikemikali ndani ya seli inafanyika vizuri
(metabolism). Pia husaidia katika kuunganisha taarifa za misuli. Ukosefu wa
vitamin hivi unapelekea ugonjwa wa beriberi ambopo mtu anakosa hamu ya kula.
Misuli kukaza pia ni dalili ya upungufu wa vitamin hivi. Wakati mwingine moyo
kushindwa kufanya kazi ni kutokana na upungufu wa vitamin hivi.
Vitamin B2 hivi
hupatikana kwenye nyama, maini, nafaka na hamira. Husaidia katika ufanyikaji wa
michakato ya kikemia ndani ya seli (metabolism). Kupasuka kwa midomo ni dalili
ya ukosefu wa vitamin hivi
Vitamin B3 hupatikana kwenye samaki, karanga,nyama, mchele
usio kobolewa na hamira.. huhitajika kwa ajili ya kuwasaidia enzymes
kubadilimchakula kuwa energy. Pellagra ni ugonjwa unaotokana na upungufu wa
vitamin hivi. Mgonjwa anakosa hamu ya kula, misuli kukosa nguvu na kuharibika
kwa ngozi.
Vitamin B6 hivi hupatikana kwenye nyama,
mbogamboga,hamira,nafaka. Husaidia katika mchakato wa protin (protein metabolism).
Ugonjwa wa anaemia, nerve irritability na vidonda kweye midomo husababishwa na
upungufu wa vitamin hivi.
Vitamin B12 hivi hupatikana kwenye samaki,nyama, mayai,maziwa
na maini. Husaidia katika utengezaji wa damu, na utengezaji wa genetic
meterials. Ugonjwa wa anaemia, upungufu wa uzito na nerve damage hutokana na
upungufu wa vitamin hivi.
Vitamin C hivi hupatikana kwenye matunda yenye uchachu kama
limao na machungwa. Mboga za kijani,na nyanya. Husaidia mwili kufyonza madini
ya chuma. Kukosa nguvu za misuli,na maumivu ya viungio(joints)kutokwa na damu
kwenye mafinzi kuchelewa kupona kwa vidonda na kuumwa mara kwa mara ni dalili
ya upungufu wa vitamin hivi.
Vitamin D hupatikana kwenye mayai, maziwa, samaki na maini.
Husaidia katika kukuwa na kuimarisha meno na mifupa. Ugonjwa wa matege kwa
watoto na osteoporosis yaani mifupa kuwa milaini husababishwa na upungufu wa
vitamin D.
Mitamini E hupatikana kwenye alizeti, butter, mchele na
peanuts. Husaidi akatika kulinda utando uliopo ndani ya mwili. Mfumo wa fahamu
kutokuwa katika hali ya kawaida ni dalili ya upungufu wa vitamin E
Vitamin K hupatikana kwnye maini na mboga za majani. Husaidia
katika kuganda kwa damu baada ya kupata jeraha. Damu kutoka kwa wingi baada ya
jeraha ni upungufu wa vitamin K.