Alhamisi, 19 Oktoba 2017

ILINDE AFYA YA MACHO YAKO

         ILINDE AFYA YA MACHO YAKO
Ugonjwa wa macho ni katika magonjwa leo yanayosumbuwa sana. Yanasumbuwa watoto wazee na vijana. Tatizo hili limekuwa likisumbuwa pia wanafunzi. Watu wengi leo wamekuwa wakitumia miwani kwa ajili ya kuwawezesha kuona. Kuna wenye  matatizo ya kutokuona ,bali na wapo wenye matatizo ya kutokuona karibu. Wengine macho yanatowa machozi na kuwasha sana. Macho kuwa mekundu na maumivu makali ni katika baadhi tu ya matatizo ya macho.

Wataalamu wa afya ya macho bado wanajitahidi kutafuta vyanzo halisi vya matatizo haya. Kwa kiasi wamefanikiwa na tiba zinatolewa kwa wenye matatizo haya. Japo kuna magojwa mengine ya macho bado haijatambulika ninini chanzo halisi lakini bado tiba zinatolewa. Wapo wanaopata matibabu kwa wajuzi wa dawa za mitishamba na wapo wanaopata matibabu kutoka hospitali.


Miongoni mwa vyanzo vya matatizo haya ni pamoja na vyakula, mashambulizi ya virusi, bakteria na fungi. Pia mabadilizo ya hali ya hewa na mazingira tunayoishi yamekuwa ni vyanzo vya matatizo ya macho kwa kiasi kinachotambuliwa. Halikadhalika matumiizi ya vifaa vya kielectronik yamekuwa ni sababu ya kupata matatizo ya macho. Baadhi ya shughuli za kibinaadamu ambazo tunazifanya kwa ajili ya kupata risiki pia zimekuwa ni katika vyanzo vya matatizo ya macho.

Miongoni mwa vyanzo hivyo vinavyosababisha matatizo ya macho lishe tunayokula imekuwa ni sababu pia. Wataalamu wa afya wanatueleza kuwa tatizo la kutokuona usiku husababishwa na upungufu wa vitamin A. vitamin hivi hueza kupatikana katika mboga za majani, maziwa, maini, karoti na machungwa. Pia itambulike kuwa mwili ukikosa vitamin A kwa kiwango kinachotakiwa ni rahisi kuathiriwa na mashambulizi kama maradhi.

Mtu mwenye matatizo haya ya kutokuona usiku inashauriwa ale sana mboga za majani ili apate vitamin A. ulaji wa karoti ikiwa imepikwa au kutengenezwa juice au ikiwa mbichi, ni muhimu. Mtu mwenye tatizo hili pia akawaone wataalamu wa afya wampatie dawa huenda akapona kwa urahisi. Pa vitamin A husaidia katika mfumo wa respiration.

Matumizi ya vifaa vya kielectronik (electronic devices) yamekuwa ni tatizo kwa macho ya watumiaji.  Mionzi itikayo kwenye vifaa hivi huwa sio mizuri kwa afya. Kwa upande wa afya ya macho si jambo la ajabu kuambiwa kuwa mwanga wa simu nao ni tatizo leo. Ukweli ni kuwa mtumiaji wa simu anatumia muda mwingi kuangalia kioo cha simu yake. Hali hii ikiendelea kwa muda mrefu inapelekea matatizo kwa afya ya macho.


Ni vizuri kupunguza mwanga wa simu hasahasa wakati wa usiku. Pia inashauriwa kukopesakopesa macho pindi unapoangalia kioo cha simu yako au kompyuta kwa muda mrefu. Jaribu kutumia miwani kwa ajili ya kupunguza nguvu za mwanga wa kioo cha kifaa chako. Weka mbali kioo cha kifaa chako na macho yako. Tumia night mode kama ipo kwenye kifaa chako.