UTANGULIZI
Sifa njema zinamstahikia Allah Mola wa ulimwengu. Rehma na amani zimshukie mtume wa Allah (s.a.w). Ama baada ya utangulizi huu mfupi, huu ni mwendelezo wa darsa za dua. Hapa utajifunza kuhusu watu ambao dua zao ni zenye kukubaliwa. Pamoja na kutekeleza taratibu zote za dua ila kuna watu ambao wakiomba dua zao huwa hazirudi.
Unaweza kupata darsa zote za dua kupitia simu yako ya kiganja. ingia play store kisha andika darsa za dua. au >>bofya hapa>> kudowanload App usome dua mbalimbali.
Tumeona katika darsa zilizopita kuhusu adabu za kuomba dua bofya hapa kusoma pamoja na fadhi la za dua bofya hapa kusoma na mengine. leo tutaona nyakati ambazo ni mahususi kuomba dua.
HALI AMBAZO MTU AKIOMBA DUA ITAJIBIWA.
1.Dua ya kumuombea aliye mbali.
Chukulia mfano una ndugu yako yupo nchi nyingine ama mji mwingine kisha ukamkumbuka na ukataka kumuombea dua, basi dua hii itajibiwa tu. Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema “hakika dua iliyo nyepesi (na haraka ) kujibiwa ni dua ya mtu kumuombea aliye mbali” (amepokea Abuu Daud na Tirmidh kwa isnad sahihi).
Pia amesimulia Abuu Dardaa رضىالله عنه kuwa mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema “dua ya mtu muislamu ni yenye kujibiwa anapomuombea ndugu yake aliye mbali. Juu ya kichwa chake kuna Malaika anaitikia ‘aamiin’ na wewe upate mfano wa wake”. (amepokea Ahmd na Muslim).
2.Dua ya mzazi, msafiri na mwenye kudhulumiwa.
Hali za watu watatu hawa wakiomba dua Allah atajibu dua zao bila ya shaka. Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema
" ثَلاَثُ دَعَوَاتٍ يُسْتَجَابُ لَهُنَّ لاَ شَكَّ فِيهِنَّ دَعْوَةُ الْمَظْلُومِ وَدَعْوَةُ الْمُسَافِرِ وَدَعْوَةُ الْوَالِدِ لِوَلَدِهِ.“dua za watu watatu (hawa) ni zenye kujibiwa na hakuna shaka juu ya hili: dua ya mzazi, msafiri na mwenye kudhulumiwa”. (amepokea Abuu Daud, Ahmad na Tirmidh kwa sanad sahihi).
3.Dua ya mwenye swaum (funga), imamu muadilifu, na mwenye kudhulumiwa.
Watu hawa dua zao zitajibiwa tu, kingozi muadilifu, mtu aliyekuwa kwenye funga na kabla hajafuturu na mtu aliyedhulumiwa. Amesema Mtume صلّي الله عليه وسلّم watu watatu dua zao hazirudi: mwenye funga mpaka afutauru, imamu muadilifu (kiongozi muadilifu), na mwenye kudhulumiwa.…….” (amepokea tirmidh kwa isnad sahihi).
ALLAH ANAJUA ZAIDI
Unaweza kusoma darsa zote za dua katika simu yako ya kignja bofya hapa. In Shaa Allah panapo majaaliwa tutawaletea darsa za qurani pamoja na tajweed. tunanamuomba Allah atupe wepesi juu ya hili. pia tunathamini mchango wenu ndugu wasomaji pindi utakapoona kosa lolote katika darsa zetu tunaomba utuelekeze ama kama una jambo unataka kuchangia tafadhali wasiliana nasi kwa namba +255712939055 kama hautatupata tutumie sma kwa nmba hiyohiyo au barua pepe rajabumahe@gmail.com.ALLAH ANAJUA ZAIDI
UHIMU KWA AJILI YAKO
Jifunze zaidi kuhusu Afya yako na lishe ukiwa na program zetu kwenye simu yako ya kiganja. bofya link zifua tazo kupata elimu zaidi juu ya afya yako
1.Afya na lishe bofya hapa
2.afya yako. bofya hapa
3.kupata post zetu moja kwa moja . bofya hapa
NYINGINEZO
1.Afya na lishe bofya hapa
2.afya yako. bofya hapa
3.kupata post zetu moja kwa moja . bofya hapa
NYINGINEZO
>>>Soma hadithi tamu za Alif Lela U Lela. bofya hapa
>>>Pata dua mbalimbali. bofya hapa
>>> Jifunze kutamka maneno ya kiingereza. bofya hapa
>>>Pata dua mbalimbali. bofya hapa
>>> Jifunze kutamka maneno ya kiingereza. bofya hapa