Jumamosi, 7 Aprili 2018

HADITHI ZA ALIF LELA U LELA (sehemu ya tatu).


ILIPOISHIA
Pale yule mzee mwenye mbuzi akajitupa miguuni mwa jini kisha kwa hisia kubwa kamwambia “ewe mkuu wa majini wa eneo hili, naomba usikiklize hadithi yangu na huyu mbuzi nilyekuwa naye hapa. Kama utaiona inastaajabisha kuliko tukio hadithi ya mwanao na mfanya biashara huyu, iwe kama fidia ya kupunguzia adhabu:.  Jini lifafikiri kwa muda na kisha likasema “vizuri sana ebu tuangalie hadithi yako”. Basi mzee yule akaanza kusimulia hadithi yake kama ifuatavyo;-
sasa endelea
    HADITHI YA MZEE WA KWANZA NA MBUZI WAKE
Mkuu sasa nakwenda nakwenda kukuhadithia habari ya ngu na huyu mbuzi niliye naye. Kwanza tambua huyu mbuzi unayemuona hapa ni mke wangu wa ndoa niliyeishi naye kwa muda wa miaka 30 bila ya kupata mtoto. Pale nyumbani kulikuwa na mtumwa hivyo nikamfanya mwanangu kwa maandishi.Mke wangu kumbe kitendo hiki hakukipenda kitendo kile. Nilitoka kwa ajili ya shughuli za kibiashara huyu mke wangu alijifundisha uchawi na akambadili mtoto wangu na mama yake kuwa ng’ombe. Kisha akawapeleka kwa mfanya kazi wangu wa shambani ili awalishe na kkuwatunza.

Haikupita muda nikarudi kutoka safarini kwangu, na nikamuuliza kuhusu mtoto wangu na mama yake lakini akanijibukuwa mama wa mtoto wangu amefariki inapata miezi miwili sasa. Na kuhusu mtoto wangu ametoweka nyumbani na hafahamiki alipo. Jambo hili lilinishangaza sana lakini sikuwa na la kufanya zaidi ya kumtafuta bila ya mafanikio.

Ulipofika msimu wa sikukuu nilimwambia mfanyakazi wangu aniletee ng’ombe aliyenona ili nimchinje kwa ajili ya kusherehekea sikukuu. Nililetewa ng’ombe mmoja mzuri sana mwenye afya. Jambo lililonishangaza wakati nataka nimchinje ng’ombe huyu alikuwa akitoa machozi na akiniangalia kwa huruma. Kwakweli jambo hili halijawahi kutokea. Nikaagizwa arudishwe na niletewe mwengine.Mkewangu alikasirika kuona ng’ombe anarudishwa, akanifata na kunisisitiza nimchinje. Nikamweleza mfanyakazi wangu amchinje yeye mii siwezi. Basi akamchinja ng’ombe yule. Jambo la ajabu ni kuwa ijapokuwa ng’ombe yule alikuwa amenenepa lakini hakuwa na nyamba ila ni mifupa mitupu. Nilishangazwa sana. Nikaagiza niletewe mwengine, na akaletwa ndama mmoja aliyenenepa vizuri. Huyu pia alifanya kama yule wa mwanzo alikuwa akitowa machozi na akajilaza miguuni mwangu kama anaomba aachiwe asiuliwe.

Huruma ilinijaa na nikaamua aondolewe aletwe mwingine. Mke wangu akanilazimisha ili nimchinge. Nikamuweka vizuri ili kuanza kumchinja, niliweka kisu kooni na nilipokaribia kumchinja aliniangalia kwa jinjo la unjonge na huku akitowa machozi. Kisu kilianguka na nikashindwa kumchinja. Nikaagiza arudishwe. Mke wangu alikasirika sana lakini mara hii sikubadili kauli yanngu

Siku ilofata mfanyakazi wangu alinifata kwa mazungumzo ya faragha akanieleza kuwa binti yake ana taaluma ya uchawi hivyo anataka kuzungumza na wewe faragha. Ilibidi nikutane nae, mazungumzo yake yaninistaajabisha sana. “mkuu ulipoondoka mkeo alijifunza uchawi na akambadili mtoto wako na yule mama yake kuwa ng’ombe. Yule ulomchinja jana ni mama yake na yule ng’ombe mdogo ulomrudisha ndiye mwanao. Nitaweza kumrudisha mwanao kawaida kwa masharti, kwanza uniwachie mkeo nimpe adhabu, na pili uniozeshe mwanao.” haya yalikuwa maneno ya binti wa mfanyakazi wangu. Nilikubaliana na masharti yale.

Yule binti akachukuwa maji na akatamka maneno nisiyoyajuwa kisha akammwagia yule ng’ombe, papo hapo akawa katik umbo labinadamu. Nilifulahi sana. Kama mashart tulokubaliana alimfata mke wangu na kutamka maneno flani na mke wangu akageuka kuwa mbuzi huyu ambaye unamuona.

Ni muda mrefu sasa hatujaonana na mwanangu hivyo nimetoka ili kama nitaweza kupata taarifa zake zozote. Hivyo nimeona ubaya kumuacha mke wangu huyu mbuzi chin ya uangalizi wa watu wengine. Nikaona bora nimchukuwe. Hii ndio stori  yangu ewe mkubwa katika majini.

“naam nakubaliana na stori yako, kweli inasikitisha hivyo nitampunguzia adhabu huyu mtu” ni maneno ya jini akimwambia mzee wa kwanza. Baada ya huyu mzee wa kwanza kuzungumza, mzee wa pili akapiga magoti kwa lile jini akaliambia, “ewe mkuu katika majini naomba usikilize na mimi stori yangu na hawa mbwa wawili, kama utaona inasikitisha zaidi naomba umpunguzie adhabu huyu mtu”. 
   

       HADITHI YA MZEE WA PILI NA MBWA WAWILI WEUSI
Mzee wa pili akapewa ruhusa ya kusimulia stori yake na mbwa wawili weusi. “kwanza utambue ewe mkuu wa majini kuwa hawa mbwa unaowaona ni ndugu zangu wa baba na mama mmoja, stori ilikuwa hivi” ITAENDELEA
kusoma hadithi hii zaidi utaipata kwenye program zetu za simu ya mkononi au bofya hapa  kusoma hadithi hizi kwenye simu yako ya kiganja bila ya kuhitaji internrt.


UHIMU KWA AJILI YAKO
Jifunze zaidi kuhusu Afya yako na lishe ukiwa na program zetu kwenye simu yako ya kiganja. bofya link zifua tazo kupata elimu zaidi juu ya afya yako
1.Afya na lishe bofya hapa
2.afya yako. bofya hapa
3.kupata post zetu moja kwa moja . bofya hapaNYINGINEZO