Jumatatu, 2 Aprili 2018

FADHILA ZA KUOMBA DUA

DUA
Sifa njema zinamstahikia Allah Mola wa ulimwengu. Rehma na amani zimshukie mtume wa Allah (s.a.w). Ama baada ya utangulizi huu mfupi, huu ni mwendelezo wa darsa za dua sehemu ya pili. hapa utajifunza kuhusu adabu za kuomba dua. itambulike kuwa dus yenye sifa za kukubali wa na Allah ni lazima zifate taratibu zilizowekwa na adabu zake. unaweza kupata darsa zote za dua kupitia simu yako ya kiganja. ingia play store kisha andika darsa za dua. au >>bofya hapa>> kudowanload App usome dua mbalimbali.


Kwa ufupi dua ni kumuomba Allah akuondoshee lililobaya, ama linalo kuudhi ama akupe jambo fulani. Na dua ni ibada kama ibada nyingine.

Dua ni jambo lenye kupendeza kama walivyosema maulamaa na masalafi wema walotangulia. Umuhimu wa dua na msisitizo wake unapatikana katika quran na sunnah.

Dua zimesisitizwa sana katika quran na sunnah hata mtume akasema لِيَسْأَلْ أَحَدُكُمْ رَبَّهُ حَاجَتَهُ حَتَّى يَسْأَلَهُ الْمِلْحَ “na aombe mmoja wenu haya yake (dua) kwa Allah mpaka chumvi.…”. Hivyo si kuomba mambo kakubwa tu na matatizo tulonayo ila mpaka chumvi. soma zaid


                FADHILA ZA DUA
1.Dua ni ibada. Basi utambue ewe ndugu muislamu kuwa dua ni ibada. Imepokewa hadithi kutoka kwa Nuuman Ibn Bashir  رضىالله عنه kuw Mtume wa Allah صليالله عليه وسلم amesema "‏ الدُّعَاءُ هُوَ الْعِبَادَةُ“hakika dua ni ibada” (imepokewa na Tirmidh na ameisahihisha).2.Dua ndio jambo tukufu zaidi kwa Allah kama Mtume صليالله عليه وسلم aliposema katika hadithi iliyosimuliwa na Abu Huraurah رضىالله عنه kuwa Mtume amesema “hakuna kitu kitukufu mbele ya Allah kuliko dua” (imapokewa na tirmidh, imam Ahmad na Alhaakim kwa isnad sahihi)
لَيْسَ شَيْءٌ أَكْرَمَ عَلَى اللَّهِ تَعَالَى مِنَ الدُّعَاءِ 

soma zaid
3.Allah anamchukia mtu ambaye hamuombi. Abuu Hurairah  رضىالله عنه amesema kuwa Mtume صليالله عليه وسلم amesema "‏ مَنْ لَمْ يَسْأَلِ اللَّهَ يَغْضَبْ عَلَيْهِ ‏"
“mtu yeyote ambaye hamuombi Allah, Allah humchukia mtu huyo” (amepokea hadithi tirmidh)


4.Allah anapenda kuombwa. Katika masimulizi ya Ibn Mas’ud رضىالله عنه Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema “muombeni Allah katika fadhila zake, hakika Mwenyezimungu Mtukufu (غزّ وجلّ) anapenda kuombwa” (amepokea Tirmidh). 
bofy hapa kusoma darsa zote.


5.Dua ni malango wa rehema. Katika masimulizi ya ibn ‘Umar رضىالله عنه kuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema "‏ مَنْ فُتِحَ لَهُ مِنْكُمْ بَابُ الدُّعَاءِ فُتِحَتْ لَهُ أَبْوَابُ الرَّحْمَةِ وَمَا سُئِلَ اللَّهُ شَيْئًا يَعْنِي أَحَبَّ إِلَيْهِ مِنْ أَنْ يُسْأَلَ الْعَافِيَةَ ‏"‏ “mwenye kufunguliwa mlango wa dua, hufunguliwa mlango wa rehema.…” (amepokea Tirmidh).

pata darsa nzima ya dua, bofy hapa
6.Dua huondosha mabalaa na majanga. Katika masimulizi ya Ibn ‘Umar, رضىالله عنه Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema “hakika dua hunufaisha kwa (hukinga) yale yanayoshuka (yanayotokea), na yale ambayo hayajashuaka ( hayajatokea). Basi jilazimisheni na (kuomba) dua enyi waja wa Allah. soma zaidi
Allah ndiye anayejua zaidi.
unaweza kusoma darsa zaidi za dua kwenye simu yako bofya hapa
Zijue dua mbalimbali na uzisome kwa kupitia simu yako bofya hapa
soma hadithi za Alif Lela U Lela bure bofya hapa

UHIMU KWA AJILI YAKO
Jifunze zaidi kuhusu Afya yako na lishe ukiwa na program zetu kwenye simu yako ya kiganja. bofya link zifua tazo kupata elimu zaidi juu ya afya yako
1.Afya na lishe bofya hapa
2.afya yako. bofya hapa
3.kupata post zetu moja kwa moja . bofya hapa

NYINGINEZO