Jumanne, 3 Aprili 2018

HADITHI ZA ALIF LELA U LELA (sehemu ya pili)


>>bofy hapa<<

ilipoishia 
Mfugaji alifikiri atumie ule ushauri wa jogoo, asubuhi ya siku ilofata mke wa mfugaji aliendelea na vurumai lake. Mfugaji akaagiza aletewe bakora nzuri na kutekeleza ushauri wa jogoo. Mambo yakatulia nyumbani na hakuleta vurumai liole tena. Baada ya kumaliza kusimulia hadithi hii waziri akamwambia Schehra-zade “binti yangu, je unataka na mimi nitumie uamuzi wa jogoo?” Schehra-zade akamwambia baba yake “hapana baba ila mi nadhani hadithi hii hainitoshelezi kubadili uamuzi wangu”. Basi waziri baada ya mazungumzo marefu akakubaliana na maamuzi ya mwanae na kukubali kumpeleka kuwa bibi harusi kwa sultan kwa usiku uliofuata.
sasa endelea.Siku ile waziri akaenda kwa sultan kwa masikitiko na majonzi akamweleza sultan kiola ambacho kilitokea kati ya yeye na binti yake. “sultan Schehra-zade anataka kwa heshima yako awe mkeo japo kwa usiku mmoja tu. Nimejaribu kumnasihi na kumkataza kwa hali zote nilizoziweza lakini imeshindikana” ni mameno ya waziri alo,mwabia sultan. “Unajuwa fika kuwa asubhi baada ya harusi itabidi ushukuwe amri ya kumuuwa na ukishindwa na wewe pia utauliwa na kichwa chako kutundikwa.” ni mameno ya mfalme akisikika anamwambia waziri.  Baaada ya mazungumzo marefu Waziri akarudi nyumbani kwa majinzi na kumueleza binti yake ajiandae kwa harusi jiono ilofata.
Schehra-zade akamueleza mdogo wake Dinar-zade “mdogo wangu ninaombi unifanyie huenda likawa ndio la mwisho kabla sijauliwa au likanusuru maisha yangu na maisha ya mabinti wengine wa nchi hii”. Nilipi hilodada? Dinar-zade alimuuliza dada yake. Schehra-zade akaendelea kumweleza “nitakapokuwa nimeingia kwa mfalme nitamwomba ruhusa ya kuwa na wewe katika chumba kile ili nipate kukuaga kabla sijauliwa. Hivyo nikipewa ruhusa hivyo itakapofika saa 11 alfajiri niamshe kisha uliombe nikusimulie hadithi nzuri iwe kama furaha ya kuagana”. Mdogo wake akakubaliana na wazo hilo la dada yake.
bofya hapa, ujifunze dua mbalimbali


Hal ilikuwa kama hivyo na harusi ikafanyika kati ya sultan na bint wa waziri mkuu. Bibi harusi akaingia kwenye jumba la kifalme huko akakutana na sura ya sultani. Kwa madaha na manjinjo akamuomba ombi lake la kuruhisiwa kuwa na mdogo wake usiki ule katika chumba kimoja ili aweze kumuaga kesho asubhi kabla ya kuuliwa. Sultan akakubali ombi lile na kuamuru Dinar-zade aletwe na chemba maalumu ikaandaliwa ndani pale. Mambo yakawa kama hivyo usiku haukuwa mrefu kati ya mabint wawili hawa. Ilipofika lisaa limoja kabla ya kupambazuka Dinar-zade akamwambia dada yake “dada yangu kipenzi, naomba unifurahishe kwa kunisimulia hadithi nzuuri iwe kama furaha ya mwisho ya kuagana kabla ya kuuliwa” Schehra-zade kabla ya kumjibu mdogo wake akaomba ruhusa kwa sultan ili amruhusu aweze kutimiza matakwa ya mdogo wake kipenzi. “hakuna shida msimulie tuu ….”’ ni maneno ya mfalme. Hapo Schehra-zade akaanza kusikumulia hadithi kama ifuatavyo.

   HADITHI YA JINI NA MFANYA BIASHARA.
Hapo zamani kulikuwa na mfanya biashara aliyejulukana kwa utajiri mkubwa sana wa mali na watoto. Alifahamika nchi nzima na aliishi maisha ya upendo na familia yake. Alitoka sikumoja katika safari zake za kibiashara. Alikuwa amepanda farasi akiwa na mfuko uiojaa tende na maji. Alifanya biashara kwa raha na amani na kuanza kurejea baada ya miezi miwili.

Siku ya nne baada ya kuanza safari ya kurudi alpita katika jangwa lililofahamika kwa jina la uwanja wa ujinini. Jina hili lilitumika miaka mingi iliyopita na huenda sasa limesahaulika. Mfanyabiashara huyu alipopita eneo hili akaona kuna mti wenye kivuli, hivyo akaamua kuketi ili apate kula chakula. Hivyo akawa anakula tende na kutupa punde pembeni. Alifanya hivi mpaka alipo maliza kula. Karibia na mti ule kulikiwa na kijieneo chenye maji hivyo alipomaliza kula tende zake akanawa mikono na akaswali swala zake.

Wakati yupo pale ghafla kulitokea upepo mkali sana na kimbunga, vumbi lilitanda eneo lile. Upepo uliambatana na moshi kisha kukatokea jini kubwa sana. “NITAKUUWA KAMA ULIVYOMUUWA MWANAGU”
 ni maneno ya jini yaliyosikika yakimwambia mfanya biashara. Nimefanya nini mpaka ninastahili kuuwawa?” mfanyabiashara akimwambia jini. Jini likaendelea “chagua nikuuwe namna gani.… Wakati ulipokuwa unakula tende zako ukawa unatupa punje na mwanangu alipita eneo lile ukampiga na punje yako akafa papo hapo. Hivyo lazima nikuuwe kama ulivyomuuwa mwanagu”

Mfanyabiashra akaendelea kumuomba jini msamaha “nisamehe mkuu, sikukusudia kumuuwa mwanao” jini kwa hasira likawa linajibu, “hakuna msamaha wala huruma hapa nitakuuwa kama ulivyomuuwa mwanangu”. Jini likatowa upanga wake kuuweka tajari kwa ajili ya kumuuwa mfanya biashara.
bofya hapa kusoma hadithi yote


Mpaka kufika hapa Schehra-zade aligunduwa kuwa asubuhi imefika tayari na sultani anatakiwa akaswali na akahudhurie kikao cha baraza. “…. Mmmh ni hadithi nzuri sana dada nimeipenda kweli, hivi mwisho wake utakuweje?, mfanyabiashara atauliwa, au jini litamsamehe?” ni maswali aliyokuwa Dinar-zade akimuuliza dad yake Schehra-zade. “mmh ni nzuri kweli na bado huko mbele ni nzuri zaidi kama sultani ataniruhusu niishi ili kesho nikusimulie muendelezo wa hadithi hii” Schehra-zade alikuwa akimjibu mdogo wake. Sultani akamruhusu asiuliwe ali aje kuimalizia hadithi yake nzuri.

Siku ile sultani alitoka akiwa na tabashahsa na hata waziri wake alishangaa kuona sultani ametoka akiwa na tabasamu bla ya kutowa amri ya kumuuwa Schehra-zade kama ilivyo kawaida yake. Sultani alifanya kazi zake za kawaida huku akiwa na shauku la kutaka kujuwa mwendelezo wa kisa cha jini.

Usiku uliingia na ilipokaribia alfajiri, sultani hakusubiri akamwambia Schehra-zade “maliza mwendelezo wa hadithi yako, ninashauku la kuta kujuwa mwisho wake”. Basi Schehra-zade akaanza kusimulia kama ifuatavyo;-

Basi yule mfanya biashara alivyoona jini anakaribia kumkata upanga akapiga magoti na kumwambia jini “tafadhali mkuu nina neno naomba unisikilize, nina familia mkuu na nina madeni naomba unipe muda angalau nikaiage familia yangu na kulipa madeni yangu”. “Unataka nikuachie ili ukimbie?” ni jini akimjibu mfanya biashara. “hapana na ninaapa kwa Mwenyezi Mungu kuwa nitarejea hapa hapa, naweka ahadi mbele ya Mwenyezi Mungu” haya maneno aliyasema mfanya biashara.

Baada ya kufikiri jini likamuuliza “haya ni muda wa siku ngapi nikupe” naomba unipe mwaka mmoja” akamjibu. Basi jini lile likakubali kichukuwa ahadi ile na likamwacha mfanya biashara papepale na likotoweka. Mfanya biashara akaondoka akiwa na mjonzi makubwa. Alipofika kwake akaieleza familia yake yote yaliyompata.

Hakuwa na muda wa kupoteza akalipa madeni yake na kuweka akiba ya kuweza kutumiwa na familia yake pindi atakapo ondoka. Mwaka haukuwa mrefu hatimaye miezi 12 ikawadia. Mfanya biashara kwa majonzi na masikitiko akaaga familia na akaondoka kwenda kutekeleza ahadi yake. Alifika eneo la tukio na kumsubiri jini aje.

Katika hali kama hivyo akiwa amekaa kumsubiri jini katokea mzee mmoja akiwa na mbuzi wake. Alistaajabu mzee yule kuona mtu eneo lile hatari. Akmuuliza hasa yaliyomkuta kukaa eneo lile, akampa kisa kizima. Kiasha yule mzee kamwambia “nitakaa hapa hapa na mimi nishuhudie kitakacho tokea”. Punde akatokea mzee mwingine akiwa na mbwa wawili weusi. Naye akataka habari ya kilichowakuta wenzie wale mpaka wakakaa pale. Akasimuliwa kisa kizima, na yeye akabaki pale ili ashuhudie kitakacho endelea. Akaja mzee wa tatu akiwa na mbwa wake mwekundu na akapewa habari na akakaa ili aone kitakacho endelea.
bofya hapa kupata elimu ya afya na vyakula


Punde wakaona moshi uliofatana na upepo na likatokea jini kubwa lililoshika upanga mkononi mwake. Jini lile haliku msemesha yeyoye likamfuata mfanya biashara na kumwambia “simama ili nikuuwe kama ulivyo muuwa kijana wangu sasa hivi sina huruma leo”.

Pale yule mzee mwenye mbuzi akajitupa miguuni mwa jini kisha kwa hisia kubwa kamwambia “ewe mkuu wa majini wa eneo hili, naomba usikiklize hadithi yangu na huyu mbuzi nilyekuwa naye hapa. Kama utaiona inastaajabisha kuliko tukio hadithi ya mwanao na mfanya biashara huyu, iwe kama fidia ya kupunguzia adhabu:.  Jini lifafikiri kwa muda na kisha likasema “vizuri sana ebu tuangalie hadithi yako”. Basi mzee yule akaanza kusimulia hadithi yake kama ifuatavyo;- itaendelea..... au bofya hapa
>.>kusoma hadithi yote bofya hapa
UHIMU KWA AJILI YAKO
Jifunze zaidi kuhusu Afya yako na lishe ukiwa na program zetu kwenye simu yako ya kiganja. bofya link zifua tazo kupata elimu zaidi juu ya afya yako
1.Afya na lishe bofya hapa
2.afya yako. bofya hapa
3.kupata post zetu moja kwa moja . bofya hapa

NYINGINEZO