Jumatatu, 6 Aprili 2020

Darsa za Swala (sehemu ya kwanza)


     Umuhimu wa Kusimamisha
Swala Kwa mujibu wa Hadith ya Ibn Umar (r.a) tuliyoirejea mwanzoni, kusimamisha swala ni nguzo ya pili ya nguzo za Uislamu. Katika kuonyesha umuhimu wa kusimamisha nguzo hii Mtume (s.a.w) amesema: Swala ndio nguzo kubwa ya Dini (Uislamu) mwenye kusimamisha swala amesimamisha dini (Uislamu) na mwenye kuiacha swala amevunja Dini .(Uislamu)


 Katika Hadithi nyingine, amesimulia Jabir (r.a) kuwa Mtume wa Allah amesema: Tofauti yetu sisi (Waislamu) na ukafiri ni kuacha swalah. (Muslim) Pia Mtume (s.a.w) amesema: Tofauti iliyopo kati yetu (Waislamu) na wengine (wasiokuwa Waislamu) ni swala (Ahmad, Abu Daud, An-Nasai, Tirmidh) 

Kutokana na hadithi hizi, tunajifunza kuwa mtu ambaye hasimamishi swala, hatakama anajiita Muislamu si Muislamu bali ni kafiri kama makafiri wengine. Anakuwa kafiri kwa sababu amekanusha amri ya Allah iliyowazi kama inavyobainika katika aya zifuatazo: Waambie waja wangu walioamini, wasimamishe swala.(14:31)  Basi simamisheni swala, kwa hakika swala kwa waumini ni faradhi iliyowekewa nyakati makhsusi. (4:103) Na waamrishe watu wako kuswali (kusimamisha swala) na uendelee mwenyewe kwa hayo... (20:132).

Tukumbuke kuwa hawi Muumini yule anayekuwa na hiari katika kutekeleza amri ya Allah na Mtume wake kama tunavyokumbushwa katika aya ifuatayo: Haiwi kwa mwanamume aliyeamini wala kwa mwanamke aliyeamini, Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapokata shauri, wawe na hiari katika shauri lao. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hakika amepotea upotofu ulio wazi. (33:36).
 Kuendelea kusoma zaidi Daunlod App yetu ya Android Bofya hapa.