Ijumaa, 17 Aprili 2020

Maajabu ya Cheetah mnyama anayekwenda mbio zaidi kuliko wanyama wote nchi kavu.
Maajabu ya Cheetah mnyama anayekwenda mbio zaidi kuliko wanyama wote nchi kavu.
Huyu ni katika wanyama jamii ya paka, na anafanana zaidi na mnyama anayeitwa puma. Cheetah ni mnyama mwindaji kama walivyo chui, simba na mbwa mwitu. Ijapokuwa cheetah wanafanana kwa sura na maumbile lakini unaweza kutofautisha mmoja kwa mwingine kwa kutofautisha rangi za kwenye mikia yao.
Cheetah ni katika wanyama walio hatarini kwa kuuliwa kwani wapo wachache sana. Wataalamu wa wanyama na watafifi wanaeleza kuwa nchi ya Namibia ndio nchi pekee yenye cheetah wengi zaidi. Inakadiriwa cheetah wanaoishi maeneo haya wanafika 2500. Cheetah anaweza kufika uzito wa kilogramu 39 mpaka 65 (kg 29 - 65).

Tafiti zinaonesha kuwa cheetah ndiye mnyama anayekimbia kwa kasi zaidi kuliko wanyama wote wa porini. Cheetah anaweza kukimbia kwa mwendokasi wa kilomita 97 kwa lisaa (97 km/h) na anaweza kuendelea kukimbia kwa mwendokasi huu kwa umbali wa mita 300. Mwili wa cheetah hauna uwezo wa kutoa jasho hivyo anapokimbia kwa umbali huu wa mita 300 bila ya kukpata kiwindwa chake cheetah huachana nae kwa kuhofia mwili wake kupata joto ambalo linaweza kumpelekea kufa.

Wanyama hawa wanakaa kwenye makundi ya familia na mara nyingi madume wanapenda kupigana. Wanyama hawa wanapoteza asilimia 10 mpaka 13 ya vile walivyoviwinda kwa simba pamoja na fisi. Tafiti zinaonesha kuwa nusu ya mawindo yao wanafanikiwa kupata chakula. Cheetah ni katika wanyama waliop hatarini sana kwani wana windwa sana na binadamu kwa ajili ya kuuliwa. Mnyama huyu anapenda kuwinda kwenye maeneo yaliyo wazi pasiwe na miti mingia mabayo itamfanya akikose kiwindwa chake kwa urahisi.

Cheetah ni katika wanyama ambao wanaweza kuishi muda mrefu bila ya kunywa maji. Kwani anajipatia maji anayohitaji kutoka kwenye mwili wa kiwindwa chake. Pindi anapowinda humnyatio mnyama wake mpaka ukaribu wa mita 10 ndipo humkurupukia na kumkumbiza kwa mwendokasi wa zaidi sana, na hukata tamaa pindi akimkimbiza kwa umbali wa mita 300.

Kuna ukweli mkubwa juu ya maisha ya wanyama, wadudu na viumbe vingine. Mbu ni katika wadudu wenye maajabu makubwa. wadudu chungu, samaki, tembo na wanyama wengine. ukipata nafasi ya kusoma maisha ya wanyama utafurahia ukisomacho.