DALILI ZA UGONJWA WA SARATANI
Ugonjwa wa saratani hutokea pale seli
za mwili zinapokuwa bila ya mpangilio maalumu na kusababisha uvimbe. Uvimbe huu
huenda ukawa mkubwa zaidi na kusababisha uharibifu wa viungo vya mwili kama
maini ubongo na mishfupa. Uvimbe huu pia hueza kusambaa mwilini na kusababisha
vimbe mbalimbali ndani ya mwili.
Kikawaida seli ndani ya mwili
huzaliwa na baadaye huweza kufa baada ya kipindi maalumu. Kwa mtu mwenye
saratani seli hizi hazifi hivyo huendelea kukuwa bila ya mpangilio. Seli hizi
huweza kuingia kwenye mfumo wa damu na kusambazwa kuelekea sehemu zingine za
mwili na hatimaye kusambaa kwa saratani viungo vingine vya mwili.
Katika sababu za kutokea kwa saratani
ni pamoja navyakula 35%, sigara30%, mionzi ya jua 10%, virus 7%, shughuli za
kazi 4%, pombe 3%, mionzi 1% na sababu nyinginezo kwa 10%. Hivyo hapa utaona
kuwa vyakula na uvutaji wa sigara vipo katika msitari wa mbele kusababisha
ugonjwa wa saratani.
Mwaka 200 WHO wametowa ripooti
inayoeleza kuwa ugonjwa wa saratani ndio unaoongoza kwa kusababisha vifo vya
watu wengi duniani.mwaka 2004 watu milioni 7.4 wamefariki kwa ugonjwa wa
saratani ambayo ni sawa nsa 13% ya vifo vyote vilivyotokea duniani mwaka huu.
Saratani ya maini, tumbo, utumbu na saratani ya matiti ndo zimeongoza kwa vifo
vya watu duniani. Vifo vinavyosababishwa na saratani
vinatarajiwa kuongezeka kila siku na vinatarajiwa kufikia milioni 12 ifikapo
mwaka 2030. (WHO. 2009).
Dalili za ugonjwa wa saratani
hutofautiona sana kulingana na aina ya saratani ambayo mtu anayo. Zipo aina
zingine za saratani hazioneshi dalili zozote mpaka zitakapokuwa zimeenea vizuri
mwilini. Ingawa hali ipo kama hivyo lakini wataalamu wa afya wameonesha baadhi
ya dalili ambazo zinaonekana kwa watu wengi wanaopata saratani ambazo ni;-
1. Homa;
Haya ni maumivu ya kishwa
yasiojulikana chanzo chake. Maumivu haya sio ya ugonjwa wowote wenye kuonekana,
hata mgonjwa akipimwa huenda asikutwe na kitu chochote .maumivu haya ni yenye
kuendelea kwa muda mrefu
2. Uchovu;
Huu ni uchovu ambao hauishi katu.
Hata mtu apate muda wa kupumzika lakini katu uchovu huu hautaondoka. Japo
mgonjwa wa kisukari pia hupata uchovu kama huu lakini saratani ina uchovu wa
kipekee. Hivuyo ni vizuri kumuona daktari akwambie aina ya uchovu ulonao.
3. Mabadiliko katika mfumo wa chakula;
Mabadiliko haya ni pamoja na
kushindwa kumeza chakula au kukosa choo. Dalili hizi huenda zikafanana na
magonjwa mengine, hivyo ukiona mabadiliko haya wahi ukamuone daktari.
4. Kushindwa kupumua vizuri;
Saratani ya mapafu huweza kuonesha
dalili hii ya kushindwa kupumuwa vizuri. Hii hutokea pale ambapo kuna vimbe sa
saratani katika mfumo wa upumuaji. Inaweza kuwa kwenye mapafu au koo.
5. Kikohozi;
Hiki ni kikohozi ambacho sababu yake
hasa ni ngumu kujulikana. Kikohozi hizi hakisikii dawa yoyote na ni chenye
kuendelea. Saratani katika mfumo wa upumuaji kama mapafu huweza kuonesha dalili
hii
6. Mabadiliko katika ngozi;
Hapa ngozi inaanza kubadilika rangi.
Pia vimbe ndani ya ngozi huanza kutokea. Madoa meupe kwenye ngozi, mdomo, na
kwenye ulimi. Pia mtu anaweza kuwa na makovu ambayo hayaponi.
7. kutokwa na damu;
Damu zinaweza kutoka katika maeneo
mbalimbali kama vile sehemu ya haja kubwa na haja ndogo kwa wanaume na
wanawake. Pia damu huweza kutoka kwenye matiti ambayo ni dalili ya saratani ya
matiti.
8. Uvimbe kwenye matiti na korodani;
Huu ni uvimbe usio wa kawaida ambao
unaanza kukuwa kwnye matiti kama dalili ya saratani ya matiti. Wakati mwingine
ngozi ya matiti inakuwa ngumu. Hali hii pia hutokea kwenye korodani ambapo
kunatokea uvimbe usio wa kawaida. Vimbe hizi pia huweza kusababishwa na mambo
mengine hivyo hakikisha unamuona daktari kwa mabadiliko haya.
9. Kupoteza fahamu au kifafa;
Kwa saratani ya ubongo huweza
ikamfanya mtu aweze kupoteza fahamu. Pia hutokea mtu akaanza kupata aina za
kifafa. Saratani hii hutokea pale ubongo uapotengeneza uvimbe.
Hitimisho;
Ushauri wangu ni kuwa watu waishi kwa
uangalifu kwani matibabu ya saratani ni ya gharama kubwa sana ni ni machache
hutolewa bure. Halikadhalika hospitali zinazotowa matibabu ya saratani ni
chache pia.