Lugha ya Qur-an:
Lugha iliyotumika
katika Qur-an ni Kiarabu sanifu kama tunavyojifu nza katika Qur-an yenyewe:
"Na namna hii tumekufunulia Qur-an kwa Kiarabu iii uwaonye
watu wa Makka na walio pembezoni mwake. Na uwaonye siku ya mkutano, siku isiyo
na shaka. Kundi moja litakuwa Peponi na kundi jingine Motoni "(42:7)
Kwa
nini Qur-an Imeshushwa kwa Lugha ya Kiarabu?
Walimwengu walio wengi
wakiwemo baadhi ya Waislamu wanaitakidi kuwa lugha ya Kiislamu ni Kiarabu na
Uislamu ni dini ya Waarabu. Bila shaka mawazo haya yamejitokeza kutokana na
kutoujua Uislamu kwa upeo wake. Uislamu ni Dini ya Walimwengu wote wa nyakati zote
na ni Dini iliyofundishwa na Mitume wote. Je, Mitume wote walikuwa Waarabu au
watu wote waliolinganiwa na Mitume hao na kuwafuata walikuwa Waarabu? Bila
shaka jibu litakuwa "hapana". Bali tunajifunza katika Qur-an yenyewe
kuwa Allah (s.w) amewajaalia walimwengu kuzungumza lugha mbali mbali na ni
katika ishara ya Uungu wake na utukufu wake.
"Na katika Ishara zake (zinazoonyesha uwezo wake) ni kuumba
mbingu na ardhi, na kuhitilafiana lugha zetu na rangi zenu. Kwa yakini katika
haya zimo ishara kwa wenye ujuzi." (3 0:22)
Kwa nini Qur-an
imeshushwa kwa lugha ya Kiarabu? Jibu lake linapatikana ndani ya Qur-an
yenyewe:
"Na hatukumpeleka Mtume yeyote isipokuwa kwa lugha ya watu
wake iii apate kuwabainishia. Kisha, Mwenyezi Mungu anamuacha kupotea amtakaye (kwa
kuwa hataki kufuata ujumbe uliomfikia wazi wazi) na humuongoza amtakaye. Naye
ni Mwenye nguvu na Mwenye Hekdma." (14:4)
Aya hii inatufahamisha
kuwa kila Mtume alishushiwa Wahyi kwa lugha ya watu wake ili yeye mwenyewe
apate kuwabainishia vizuri na wao wapate kumuelewa vizuri. Kwa kuwa Mtume
Muhammad (s.a.w) alikuwa Mwarabu wa kabila Ia Kiquraishi na kwa kuwa Maquraish
na Waarabu kwa ujumla ndio watu wake wa mwanzo kuwalingania Uislamu ili
wamsaidie kuufikisha ulimwengu mzima. Qur-an ilibidi ishushwe kwa lugha ya
Kiarabu cha Kiquraish kilichokuwa fasaha kuliko vilugha vyote vya Kiarabu. Watu
wake wasingemuelewa kabisa kama Mtume (s.a.w) angewalignania kwa lugha
isiyokuwa ya Kiarabu:
"Na lau kama tungalifanya Qur-an lugha isiyo ya Kiarabu
wangelisema: Kwa nini aya zake hazikupambanuliwa? Lo! Lugha isiyokuwa ya
Kiarabu na (Mtume) Mwarabu! (Mambo gani hayo)? " (41:44).
"Na lau tungaliiteremsha juu ya mmoja wa wasiokuwa Waarabu, na
akawasomea (kwa ufasaha) wasingalikuwa wenye kuamini." (2
6:198-199)
Kutokana na aya hizi tunajifunza kuwa:
(i) Ni desturi ya Allah (s.w) kumtuma mjumbe
wake kwa lugha ya watu wake anaowafikishia.
(ii) Qur-an imeteremshwa kwa lugha ya Kiarabu
kwa kuwa Mtume Muhammad (s.a.w) alikuwa Mwarabu na wale aliowalingania mara ya
kwanza walikuwa ni Waarabu.
(iii) Waarabu wa mwanzo kulinganiwa Uislamu na
Mtume (s.a.w) wasingeliukubali ujumbe kama Mtume asingelikuwa Mwarabu na kama
angelingania kwa lugha nyingine isiyokuwa ya Kiarabu.
(iv) Kama Mtume (s.a.w) angelingania kwa lugha
nyingine isiyokuwa Kiarabu, ujumbe wake usingelifahamika na watu wake
wasingelazimika kuufuata kwa kuwa hawauelewi.
Ujumbe wa Qur-an Utawafikiaje Wale wasio Waarabu au wale
Wasiojua Kiarabu?
Si jambo zuri na Si
hekima mtu kufikisha ujumbe kwa Kiarabu wakati waSikilizaji wake hawafahamu
lugha hiyo. Ni kweli kuwa Kiarabu ni lugha ya Qur-an na lugha aliyoitumia Mtume
(s.a.w) kufundishia yale aliyoteremshiwa kutoka kwa Allah (s.w). Hivyo ni lugha
ambayo inampasa kila Muislamu ajitahidi kujifunza. Pamoja na umuhimu wa kuifahamu
lugha ya Kiarabu, haina maana kuwa anayekijua Kiarabu ndiye Muislamu na yule
asiyekijua ni Muislamu mwenye kasoro.
La muhimu ni kuujua
ujumbe wa Qur-an na kuendesha maisha ya kila siku kwa mujibu wa ujumbe huo.
Ujumbe wa Qur-an unaweza kumfikia kila Muislamu pasina shaka yoyote kwa lugha
yake kwa kusoma tafsiri na sherehe ya Qur-an ambayo kwa Rehema ya Allah (s.w)
imetolewa katika lugha mbali mbali na wanachuoni wacha Mungu ambao ni mashuhuri
katika uliwengu wa Waislamu.
Tukumbuke kuwa Qur-an
imeshushwa kwa ajili ya walimwengu wote ambao Allah (s.w) amewajaalia
kuzungumza lugha zinazotofautiana (rejea Qur-an (39:22). Naye Mtume (s.a.w) pia
ameletwa kwa ajili ya walimwengu wote. Hivyo ili ujumbe wa Qur-an na Sunnah
uwafikie walengwa wote, hauna budi kufasiriwa kwa lugha za walengwa wote. Kazi
ambayo kwa Rehema ya Allah (s.w) imeshafanyika. Leo hii hapana udhuru kwa mtu
yeyote ulimwenguni wa kutoufahamu ujumbe wa Quran kwa sababu si Mwarabu au
hajui Kiarabu
Haja
ya Kujifunza Lugha ya Kiarabu kwa Waislamu:
Ipo haja kubwa kwa
Waislamu kujifunza lugha ya Kiarabu kuliko ile haja tunayoitambua ya kujifunza
lugha za kigeni na za Kimataifa kama vile Kiingereza, Kifaransa, n.k. Kwa mfano
hapa Tanzania tunajifunza lugha ya Kiingereza (English) ili tuweze kufaidika
kitaaluma, kiuchumi, na kisiasa n.k. Tukijifunza lugha ya Kiarabu tunafaidika
na hayo yote pamoja na ziada ifuatayo:
(i) Tutaufahamu ujumbe
wa Qur-an na mafundisho ya Mtume (s.a.w) kwa lugha yake ya asili. Daima tafsiri
haikosi upungufu japo kidogo.
(ii)Tutaweza kufahamu
maana ya undani ya dua na dhikiri mbali mbali tunazoleta katika ibada maalum
kama vile swala ambapo haturuhusiwi kutumia lugha nyingine isiyokuwa Kiarabu.
Kufahamu maana ya yote tuyasemayo katika swala hutupelekea kuwa na khushui
inayotakikana.
(iii)Lugha ya Kiarabu
ni chombo cha kuwaunganisha waislamu wote ulimwenguni ili wadumishe udugu na
umoja wao kama wanavyotakiwa wawe. Kama Waislamu wanavyoshikamana katika swala
kwa kutumia lugha moja ndivyo wanavyotakiwa waelewane na kushikamana katika
ibada zote zinazofanywa kimataifa kama vile Ibada ya Hijja