Mafua ni ugonjwa unaosababishwa
na virusi vya mafua na pia inasadikika
kuwa zipo takribani aina 200 za virusi hawa wa mafua wakiwemo rhinoviruses,
parainfluenza viruses, enteroinfluenza viruses na vingine vingi. Virusi hivi
hupatikana kwa kukutana na hewa yenye virusi hawa, pindi unapovuta hewa yenye
mchanganyiko wa virusi hawa. Sababu zingine zinazosadikika kusababisha mafua ni
panoja na sigara, moshi, mavumbi, baridi kuwa kali au kuchafuka kwa hewa.
Udonjwa wa mafua unadalili
tofauti tofauti na huenda zikafanana na ugonjwa wa malaria. Miongoni mwa dalili
hizo ni pamoja na kukosa hamu ya kula, kuhisi uchovu, kutokwa na makamasi
mengi, koo kukereketa, maumivu ya kichwa na kupiga chafya mara kwa mara. Japo
dalili za mafua hutofautiona kwa mtu na mtu kulingana na uwezo wa mwili wake
kupambana na magonjwa ila hizi dalili tulizozitaja huwa maarufu kwa watu wengi.
Mgonjwa wa mafua huenda akawa
amechoka sana kiasi kwamba analala kitandani kwa homa kali aliyo nayo. Mafua
huwaathiri zaidi watoto na wazee kwani miili yao haina kinga za kutosha
kupambana na maradhi. Kwa wale wenye HIV+ ugonjwa wa mafua pia hueza ukawaletea
athari kubwa sana ikiwemo homa kali na uchovu.
Mtu ana weza kujikinga na mafua
kwa kuosha mikono kabla na baada ya kula,
kuziba mdomo anapopiga chafya. Kula vyakula vyenye vitamin A na C kwa
wingi, kunywa maji mengi na kupunguza mawazo yaani ”stress” kwa lunga ya kigeni hapa kinacho maanishwa ni
kuwa na furaha. Jambo la msingi limgine ni kuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi
mara kwa mare humuepusha mtu na mafua kwa kiasi kikubwa.
Miongoni mwa vyakula anavyotakiwa
ale mwenye mafua ni kama mboga za majani
zenye vitanimi kwa wingi, kwa mfano spinach, na mchicha. Pia kula
matunda yenye vitamin C kwa wingi kama mapapai, na machungwa. Vyakula hivi
husaidia katika kuupa mwili uwezo mkubwa wa kupambana na maradhi na
mashambulizi mengine. Maji ya kutosha humsaidia mtu mwili wake kuweza kufanya
kazi ya kudhibiti maambukizi kwa urahisi. Hali kadhalika kufaya mazoezi husaidia
mwili kufanya kazi vizuri. Pia anashauriwa mgomjwa wa mafua awe chai.
Wapo baadhi ya wataalamu wa tiba
mbadala wanazungumzia matumizi ya kitunguu maji kuhusu kutibu mafua. Wanatumia
harufu ya kitunguu maji kutibu mafua. Mgonjwa atachukuwa kitunguu kasha ataondowa
majani, au maganda ya juu kisha atakuwa anavuta haruvu ya kitungu. Atafanya
hivyo kwa mara kadhaa hasa anapokwenda kulala.