Ijumaa, 20 Oktoba 2017

VIJUWE VYAKULA VYA MADINI NA FAIDA ZAKE

           VYAKULA VYA MADINI NA FAIDA ZAKE
    Kama tulivyokwisha kutaja katika post zilizopita kuhusu aina za vyakula. Leo tutakuleteeni mengi kuhusu vyakula vya madini , faida zake, vinapo patikana na magonjwa yanayohusishwa na upungufu wa madini hayo.

1.Madini ya sodiam “sodium”(table salt)  madini haya unaweza kuyapata kwenye spinach, maharage,punje za maboga n.k. madini haya ni muhimu kwa ajili ya mfumo wa fahamu, ufanyaji kazi mzuri wa mizuli, kudhibiti kiwango cha maji mwilini, utengenezwaji wa asid ya hydrocloric tumboni. Kuimarika kwa mifupa na utulivu wa mfumo wa fahamu huhitaji madini haya.
Upungufu wa madini haya utapelekea udhaifu wa misuli na udhaifu wa mifupa. Pia mapigo ya moyo kutokuenda vizuri husababishwa na upungufu wa madini haya.


2.Madini ya chuma. Haya hupatikana kwenye maini, nyama, maharage, na mboga za majani. Madini haya ni muhimu kwa utengenezwaji wa hemoglobin yaani chembechembe nyekundu za damu. Upungufu wa madini haya hupelekea matatizo katika mfumo wa damu. Ugonjwa wa anaemia unamahusiano ya moja kwa moja na upungufu wa madini ya chuma. Madini ya zink, hupatikana kwenye kamba, kaa, nyama na hamira. Husaidia pia katika afya njemaya mfumo wa kinga (immune system) na uponaji wa majeraha.
Upungufu wa madini haya hupelekea matatizo katika, ngozi, meno na mfumo wa kinga mwilini (immune system).

3.Madini ya kashiam(calcium). Haya hupatikana kwenye maziwa,maini, mboga za majani na cheese. Madini haya husaidia katika uimarishwaji wa mifupa, meno, misuli na utengenezwaji wa neva. Husaidia piaa kuwezesha kuganda kwa damu kwenye majeraha. Husaidia katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kwa kuzifanya enzymes kuwa active.
Madini haya yakipunguwa mwilini mifupa na meno huwa na udhaifu. Halikadhalika damu hutoka kwa muda mrefu baada ya jeraha kabla ya kuganda.

5.Madini ya phosphorus, haya hupatikana kwenye nyama, maziwa, samaki, na mayai. Husaidia katika uimarishwaji wa mifupa, meno,misuli na shughuli za mfumo wa fahamu na utengenezwajiwa genetic materials.

6.Potashiam (potassium) hupatikana kwenye ndizi, machungwa,nyama na kaa. husaidia katika kurekebisha kiwango cha majimaji mwilini.
Upungufu wa madini haya unaweza kupelekea matatizo katika misuli.

7.kopa ( copper) haya hupatikana kwenye nyama, samaki, na maini.husaidia katika mifupa na utengenezwaji wa hemoglobin (chembechembe nyekundu za damu).
Upungufu wa madini haya unaweza ukapelekea urahisi katika kupasuka kwa mishipa ya damu, matatizo mkatika mifupa na viungio (joints).

8.manganese madini haya hupatikana kwenye figo,maini, chai na kahawa. Husaidia katika utengenezwaji wa mifupa, na katika mmeng’enyo wa chakula kwa kufanya enzymes ziwe active.
Upungufu wa madini haya unaweza ukapelekea kupoteza kwa joto mwilini, mifupa kuwa nyepesi, kutokwa na damu za pua na kupata kizunguzungu.

9.iodine madini haya hupatikana kwenye chumvi na vyakula vya baharini kama samaki. Husaidia katika uzalishaji wa homoni ya thyroid. Ugonjwa wa goita (goiter) husababishwa na upungufu wa madini haya.