YANAYOPUNGUZA KINGA YA MWILI WAKO.
Upungufu wa kinga huonekana pale mwili unaposhindwa kupambana na maradhi na wadudu shambulizi. Upungufu huu wa kinga huenda mtu akazaliwa nao au akaupata katika maisha kadri anayokuwa. Itambulike kuwa si kila upungufu wa kinga ni sababu ya HIV au UKIMWI hapana. Mtu ataambiwa ana HIV pindi seli zake ya cd4 zinapokuwa chini ya 500 katika mililita moja ya ujazo.
Mfumo wa kinga mwilini ni unatengezwa na organ mbalimbali kama vile;-
1.bone marrow ni ujiuji unaopatikana kwenye mifupa
2.Tonsils
3.Spleen
4.lymph node
Ogan hizi ndizo zinahusika na utengenezwaji wa lymphocite yaani seli nyeupe za damu. Seli hizi ndizo zenye kazi ya kupambana na maradhi yote mwilini. Pia hizi ndizo zinazopambana na vijidudu shamulizi ambavyo ni
1.Bakteria
2.Virusi
3.Fangas(fungi)
4.Seli za saratani
Mfumo wa kinga mwilini unaweza kudhuriwa na mambo mengi sana. Miongoni mwayo ni;-
1.kutokufanya mazoezi ya kutosheleza afya ya mwili. Hapa itambulike kuwa mtu anaweza akawa anafanya mazoezi, lakini yakawa mazoezi yale si yenye kutosheleza. Angalau kiafya mtu ajitahidi apatejasho. Pia ni vizuri kuvaa tracksut na vi vyema jasho likakaukia kwenye nguo hii. Kitendo hiki husaidia kupunguza mafuta mwilini.
2.Misongo ya mawazo yaani stress. Msongo wa mawazo husababisha kuuwa seli za mwili na kudhoofisha mfumo mzima wa afya na kinga mwilini kwa muda mchache sana. Mtu anatakiwa ajitahidi kuwa na furaha au kuitafuta furaha kwa namna yoyote ile. Itambulike kuwa msongo wa mawazo ni katika vyanzo vikuu vya vidonda vya tumbo. Maumivu ya tumbo pia huweza kusababishwa na misongo ya mawazo.
3.Kujosa muda wa kutoka kulala. Kukosa usingizi ni katika mambo hatari sana kiafya. Mtu anatakiwa apate muda wa kutosha wa kulala ili kuuwezesha mwili kufanya shughuli zake za ndani kwa usahihi na utaratibu ulio salama. Pia kukosa udingizi kunaweza kusababisha maumivu ya kichwa. Halikadhalika uwezo wa akili na mwili kufanya kazi unaweza kudhurika kwa kiasi kikubwa.\
4.Mfumo mbovu wa kula. Mtu anatakiwa ale kiutaratibu na ale mlo kamili. Vyakula vya mafuta havitakiwi kuvila kwa wingi. Mtu anatakiwa ale na afanye mazoezi. Magonjwa mengi anayouguwa mwanadamu ni kutokana na vyakula anavyokula. Ulaji wa nyama uwe katika mpangilio mzuri. Pia itambulike kuwa zipo nyama zinadhuru afya kama vyama ya nguruwe. Mtu ajitahidi kuala samaki, matunda na mboga za majani kwa kiasi kikubwa kuliko nyama nyekundu.
>>bofya hapa kupata update zetu<<
>>bofya hapa kupata update zetu<<